Uamuzi mpya wa kufunga
mpaka sio uamuzi pekee uliochukuliwa na Burundi. Waziri wa utawala na usalama
nchini Burundi, Martin Nigetes, katika mkutano na mamlaka katika jimbo la
Kayanza, alisema kuwa Wanyarwanda hawahitajiki nchini Burundi.
Akasema: “...Hatuhitaji watu wao wenyewe, na wale waliokuwa hapa kwenye ardhi hawatakikani”.
Warundi na Wanyarwanda waliozungumza kuhusu uamuzi huu walionyesha kuwa ingawa mamlaka ya Burundi ina sababu za kuchukua uamuzi huu, wanaona kuwa ni hatua ya kurudi nyuma
Mwaka mmoja uliopita, Mrundi Aimé Claude Nkurunziza alianzisha upya biashara kati ya Kigali na Bujumbura kupitia njia ya ardhini, baada ya miaka mingi ya kutofanya kazi kwa sababu ya hali ya uhusiano kati ya serikali hizo mbili.
Wakazi mbalimabli
wanaoishi jirani na mipaka ya nchi hizo mbili wakingea na vyombo mbalimbali vya
habali wamesema kuwa:
"Mambo yalianza
kwenda vizuri, sasa tazama. Hii haifaidi mtu yeyote, usalama ni sawa, lakini
serikali zote mbili zinajali jinsi tunavyoishi. Nadhani haitakiwi kufungwa tena.”
Honorine Gatesi, anayeishi katika jiji la Huye kusini mwa Rwanda, pia anasema karibuni alianza kusafiri hadi Ngozi nchini Burundi kuwatembelea wanafamilia wake.
Aidha Honorine
ameongeza kwa kusema kuwa “Sasa mimi pia nimenyimwa haki ya kuwatembelea binamu
zangu, hawawezi kuja hapa na hatujui hii itachukua muda gani. Imepita zaidi ya
miaka mitano tangu tulipowaona jamaa zetu mara ya mwisho. Ni jambo la
kusikitisha.
0 Comments