MAWAKALA WA MABASI WA STENDI KUU MISUNA SINGIDA WACHANGIA MIFUKO YA SARUJI HANANG.

 

Mwenyekiti wa Umoja wa Mawakala Wa Mabasi Mkoa wa Singida Msafiri Ndui akisain kitabu  cha wageni katika 
Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Hanang.


                                      Picha ya kumbukumbu baada ya kusaini kitabu cha wageni.

               Baada ya kusaini kitabu cha wageni wakipiga picha na Afisa Utumishi wa Halmashauri ya  hiyo.


                                           Mifuko ya Simenti iliyokabidhiwa kwa waathilika wa Mvua hizo. 


Ni katika kijiji cha Jorodon baada ya kukabidhi msaada tukiwa na Mh Dc wa Stendi Misuma anaitwa Mamy.


                                              

                                                  Barabara ya kwenda kwa Mhe Merry Nagu kiijini Jorodon




Wajume na Viogozi wa Umoja wa Mawakala wakitazama eneo la kitongoj cha Joromon lilivyo athilika na Maporomoko hayo. 

                                                 

                                              Bonde la chanzo cha maji katika kijiji cha Jorodon.


Tulikutana na Taasisi ya dini ya Kislam ikiongozwa na mashekh kutoka mkoaani Singida na kupata fulsa ya kuwaombea dua wenzetu waliyotangulia mbele ya haki





Umoja wa Mawakala wa Mabasi ya abiria yanayofanya safari za mikoani stendi kuu Misuma Singida mjini umetembelea wilaya ya Manyara katika Halmashauri ya Hanang Katesh mjini kwa lengo la kuunga mkono kauli ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan alipofika wilayani hapo baada ya mafuliko yaliyo sababishwa na mvua kubwa iliyoleta maafa makubwa  na kusababisha vifo na wengine kupoteza makazi yao.

Mwenyekiti wa Umoja huo Msafiri Ndui Akiongea na wanahabari katika kitongoji cha Jorodon  amesema kuwa wao kama umoja wa Mawakala wa Mabasi Misuna Singida wanatoa pole kwa ndugu na jamaa waliyopoteza mali zao katika maafa hayo na kuchangia mifuko amsini (50) ya Saruji kwajili ya Ujenzi wa nyumba za makazi kwaajiri ya waathirika wa janga hilo.

 Aidha makamu mwenyekiti wa Umoja huo Salihina Kajuna amewataka watanzania kuunga mkono jitihada za Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan huku akiwaomba wanaumoja katika Stendi mbalimabli nchini kutoa misaada kwa wenzetu Hawa waliyo poteza mali zao.

 Naye Mkuu wa Wilaya ya Hanang Janeth Mayanja baada ya kupokea mifuko hiyo (50) ya Simenti amewashukuru Mawakala hao nakusema kuwa pamoja na kazi ngumu wanazofanya Mawakala hao lakini wamekua ni mfano wa kuigwa na Kazi ya maandalizi ya Ujenzi wa nyumba za makazi inakwenda kuanza Mara moja kwani eneo lipo tayali na vifaa vipo pia kama Serikali ilivyosema.

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments