Afisa Kilimo wa wilaya ya Ikungi Gurisha Msemo akitoa taarifa ya kilimo ya wilaya kwa Mkuu wa Mkoa Singida.
Viongozi wa ngazi ya Wilaya hiyo wakifurahia jambo katika kikao kazi hicho kilicho fanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi.
Wakulima wilayani ikungi
wametawa kuhakikisha wanatumia vyema mbolea ili kupata mazao zaidi katika
mavuno yao na kuinua pato la familia na Taifa.
Kauli hiyo imetolewa na
mkuu wa mkoa wa Singida Peter Serukamba wakati akiongea na maafisa
ughani,madiwani na wakuu wa idara mbalimbali kutoka ofisi ya Halmashauri
ya wilaya hiyo.
Serukamba amewaagiza
madiwani wote wilayani humo kwenda kufanya mikutano na wananchi kwa lengo la
kutoa elimu juu ya matumizi bora ya mbolea.
Naye afisa kilimo wa
wilaya hiyo Gurisha Msemo akitoa taarifa ya kilimo ya wilaya amesema kuwa
wamefanikiwa kuongeza ekari za kilimo 15,261 ikiwa ni agizo la Mkuu wa Mkoa
nakueleza kuwa kuwa mpaka sasa halmashauri imefanikiwa kusajili wakulima
zaidi ya 12,989 kwenye mfumo huku lengo likiwa ni wakuima 15,000 ambao
watanufaika na mbolea hiyo.
Aidha mkuu wa Wilaya ya
Ikungi Thomas Apson Amesema kuwa ili kufanikiwa na kutimiza malengo yeo lazima
wakuu wa Idara na Viongozi wa ngazi mbalimbali wilayani humo lazima waungane
katika kusimamia na kuendelea kutoa elimu kwa wananchi wa maeneo yote ili
waweze kunufaika na matumizi ya mbolea.
0 Comments