DURU LA USAJILI WA DIRISHA DOGO JAN 2024

 

                                                            Beki kisiki wa Ufaransa Jean Todibo 24

Manchester United wanatakiwa kulipa pauni milioni 52 ili kumnasa beki wa kati wa klabu ya Nice na timu ya Taifa ya Ufaransa Jean-Clair Todibo, 24, ambaye wanavutiwa na kiwango chake.(Caught Offside)

United pamoja na Chelsea wanavutiwa na mshambuliaji kinda wa Sweden Jonah Kusi-Asare mwenye miaka 16 anayecheza katika klabu AIK. Bayern Munich pia wanavutiwa na kinda huyo. (HITC)

United pia wameanza mipango ya awali kumnasa kiungo kinda wa Ubelgiji Arthur Vermeeren, 18, kutoka klabu ya Royal Antwerp. 


                                                                     Tanguy Ndombele, 27

Klabu ya Tottenham inapanga kumrejesha kiungo wake Tanguy Ndombele, 27, from his kutoka klabu Galatasaray anapocheza kwa mkopo kwa sababu ya kutokuwa na uhakika wa kumnasa Conor Gallagher kutoka Chelsea. (Football Transfers)

Italazimika Wolves kupewa “kitita cha kurusha cha pesa” ili kumuuza kiungo wao raia wa Brazil Joao Gomes, 22, katika dirisha la usajili la mwezi Januari. Tottenham wanaripoti wa kuvutiwa na mchezaji huyo. (Mirror)


                                                                      Hamed Traore, 23.

Klabu ya Napoli imetuma dau la usajili kwa kiungo wa klabu ya Bournemouth na timu ya taifa ya Ivory Coast Hamed Traore, 23. (Fabrizio Romano)

Sweden wamefanya mazungumzo na kocha wa zamani wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer juu ya uwezekano wa kuinoa timu ya taifa hilo la Scandinavia. (Fotboll Skanalen - in Swedish)

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments