MZEE ANUSULIKA KUKATWA NYETI IKUNGI.


 picha: kutoka maktaba.

MKAZI wa Kijiji cha Mtunduru Kata ya Mtunduru Wilaya ya Ikungi mkoani Singida Almasi Ramadhani Khaliki (70) amenusurika kuhasiwa na vijana 5 akitoka kunywa pombe za kienyeji kilabuni saa 2:00 usiku njiani akielekea nyumbani kwake.

Habari zilizotolewa  na Mwenyekiti wa Kijiji cha Mtunduru Juma Khambi amesema siku ya tukio hilo Mzee Almasi alikwenda kunywa walijitokeza vijana watano wakakaa karibu naye wakampa pombe waliyonunua wakaanza kunywa wote.

Vijana hao walipoona mzee ameanza kulewa wakaondoka wakaenda kumvizia njiani kwenye vichaka, mzee huyo akaondoka kwenda kwake alipofika vichakani vijana  hao walijitokeza ghafla wakamkamata kwa nguvu wakamtoa nguo wakatoboa korodani moja upande wa kushoto wakitumia kitu chenye ncha kali (kisu) huku qakidai wanataka wachukue gorori zote mbili kama walivyoambiwa na mganga wao Arusha.

Vijana hao ni Mohamed Issa (30), Salumu Shabani (32), Mahamudu Ramadhani na Hamza Ramadhani lakini Yule wa tano alikimbia na jina lake halikujulikana na yeye hajulikani alipo mpaka sasa.

Mzee Almasi alijisikia maumivu makali sana akapiga yowe na kelele akiwa amekandamizwa chini kwa bahati nzuri sehemu yenyewe watu wanapita wengi wakasikia yowe wakafika wakawakamata wawili wengine walikimbia, sehemu iliyotobolewa ilitoa damu nyingi sana.

Habari zinasema wale waliowakamata wale vijana wakatoa taarifa kwa viongozi wa kijiji na kata na watu wengine walipofika na kumuona mzee huyo katika hali ile wakawahoji wale vijana kisa cha kutaka kumuua walisema wametumwa na mganga watafute gorori mbili kutoka kwa mtu aliyezaa mapacha wakatengenezewe dawa wapate mali.

Afisa Mtendaji Kata ya Mtunduru mwakapumbila amesema vijana wale waliokimbia walikamatwa wawili lakini Yule mwingine hajulikani alipo kutokana na kutokwa na damu nyingi mzee Almasi akazinia muda ule saa 2:00 usiku, wote wakapelekwa Sepuka vijana wakapelekwa polisi na mhusika alipelekwa kituo cha Afya Sepuka.

Wale vijana wamedai wanavitaka vifaa vyote viwili wavipeleke Arusha kwa mganga wakatengenezewe dawa wapate mawe kwenye machimbo Mererani wauze wapate fedha.

Hata hivyo hali ya mzee Almasi kwa sasa inaendelea vizuri baada ya kupata matibabu kituo cha afya Sepuka na alipotakiwa na gazeti hili kutoa maelezo ya kisa chote kilivyokuwa hadi wale vijana wafikie kumkamata na kumtaka sehemu nyeti alisema walikuwa wananchi wakavitaka vyote viwili wametumwa na Mganga kutoka kwa mtu aliyezaa mapacha.

Mzee Almasi akielezea juu ya tukio hilo amesema siku ya tukio hilo alikwenda kunywa pombe klabuni kama kawaida yake na alipopombeka akaamua kurudi nyumbani kumbe njiani vichakani akashtukia akivamiwa na vijana watano na ilikuwa  saa 2:00 usiku.

“Nilishtukia nikivamiwa, nikakamatwa nikaangushwa chini wakanitoa nguo wakanikata korodani moja la upande wa kushoto nikaona maumivu makali sana nikapiga yowe na makelele watu wapiti njia walifika” alisema mzee huyo.

“Wale vijana walisema huyuhuyu ndiyo tunamtaka amezaa watoto mapacha ndiyo dawa zetu zitaenda vizuri sasa tunchukue yote mawili.” Alimasi alisema.

Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Sepuka Dkt. Kessia Mhina amethibitisha kumpokea mzee Almasi Ramadhani akiwa amezimia na sehemu moja ya korodani la kushoto limekatwa kwa kutumia kitu chenye ncha kali, waganga wakamshona nyuzi tatu na saa 12:30 jioni alizinduka na wakampa ruhusa ya kurudi kwake kesho yake baada ya kuonekana ananafuu.

Polisi wanaendelea kuwashikilia vijana 4 katika mahojiano kujua kisa hasa cha kutaka kumhasi mzee huyo na baadaye kujibu mashtaka yao yanayowakabili.

Kamanda wa Polisi Mkoani Singida Stella Mutabihirwa hakuweza kupatikan kwa simu yake kuelezea kama anazo taarifa hizo kutoka kijiji cha Mtunduru.

Mwisho.


Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments