VICTOR OSIMHEN WA NIGERIA (MVP) WA (CAF)

 Victor Osimhen wa Nigeria ametawazwa Mwanasoka Bora wa Afrika 2023 katika hafla ya utoaji wa tuzo za Shirikisho la Soka Afrika (Caf) mjini Marrakesh.

Mchezaji huyo wa Napoli aliwashinda Mmisri, Mohamed Salah na Achraf Hakimi wa Morocco katika tuzo hiyo ya kifahari - hii ikiwa ni mara ya kwanza kwa Mnigeria kutwaa taji hilo tangu Nwankwo Kanu mwaka 1999.

Nigeria ilifurahia mafanikio maradufu huku Asisat Oshoala akihifadhi tuzo ya upande wa wanawake - ikiwa ni mara ya sita kwa nyota huyo wa Barcelona kushinda tuzo hiyo.

Washindi hupigiwa kura na jopo linalojumuisha kamati ya ufundi ya Caf pamoja na wanahabari wa Afrika, makocha wakuu na manahodha. Vilabu vinavyoshiriki katika hatua ya makundi ya mashindano ya bara Afrika pia vina usemi kuhusu mshindi wa tuzoOsimhen wa Napoli, 24, alipendekezwa kutwaa tuzo ya kifahari ya Caf kwa mara ya kwanza katika maisha yake ya soka baada ya msimu mzuri wa 2022-23.

Alifunga mara 26 katika mechi 32, likiwemo bao muhimu lililoifungia Scudetto mwezi Mei na kushinda Napoli taji lao la kwanza la Serie A katika kipindi cha miaka 33.

Mshambulizi huyo wa zamani wa Wolfsburg na Lille pia alichaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Mwaka wa Chama cha Wachezaji Soka wa Italia mapema mwezi huu baada ya kuwa na msimu mzuri.

Osimhen mzaliwa wa Lagos alifunga mabao matano katika mechi nne za kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) nchi yake ilipotinga fainali mwaka ujao.

Pia alikuwa Mnigeria wa kwanza kumaliza katika 10 bora ya kura ya Ballon d'Or na kumaliza katika nafasi ya nane na akafanywa kuwa Mwanachama wa Jamhuri ya Shirikisho katika nchi yake. hiyo.


Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments