Waziri Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mohamedi Mchengerwa kiongea na Viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Singida.
wakurugenzi wa Halmshauri za wilaya za Mkoa wa Singida.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida Mather Gwau akitoa Salamu kwa niaba ya wabunge wa mkoa wa Singida.Waziri Mchengerwa akikata Utepe na viongozi wa Mkoa wa Singida.
Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskas Muragili akipokea funguo za Gari.
Wakuu wa mikoa nchini wamepongezwa kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kusimamia miradi ya maendeleo ambayo imekamilika na mingine inaendelea kukamilishwa.
Ameyasema hayo Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa katika ziara yake mkoani Singida ambapo aliweza kuzindua magari ya ufuatiliaji ya sekta ya afya pamoja na kutembelea mradi wa ujenzi wa kituo kipya cha afya kata ya Mtipa, Manispaa ya Singida kilichojengwa kwa mapato ya ndani.
Mchengerwa amezitaka Halmashauri zote nchini kuiga mfano wa Halmashauri ya Manispaa ya Singida ambayo imeweza kutumia vyema mapato yake ya ndani kwa kuwajali wananchi wake kupitia miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa makusanyo ya ndani .
Aidha amesema katika kuunga mkono mradi huo wizara yake imetoa fedha kiasi cha
Shilingi milioni 150 kwa ajili ya ununuzi wa dawa na vifaa tiba, na kutoa rai
kwa uongozi wa Mkoa na Manispaa kuhakikisha kituo hicho kipya cha afya
kinafunguliwa haraka ili kuanza kutoa huduma.
Aidha mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba amesema Jumla ya Magari 06
yamekabidhiwa kwa halmashauri 5 za Iramba, Mkalama, Halmashauri ya Wialya ya
Singida, Ikungi na Manyoni wakati gari moja likabidhiwa kwa Mganga Mkuu
wa mkoa yote ni kwa ajili ya ufuatiliaji wa shughuli za afya katika
Halmashauri.
0 Comments