MADEREVA WA MABASI 10 WAFUNGIWA LESENI

 

kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani Mkoa Singida Fenny Mashanjala na ACP Stella Mutahibirwa wakifutilia taarifa mbalimbali.


Kamanda wa Polisi Mkoa Singida ACP  Stella Mutabihirwa na Makamu mwenyekiti wa usalama mkoa Singida Fenny Mashanjala wakikata utepe kuashiria makabidhiano ya Gari hilo.


Makamu mwenyekiti wa usalama barabarani mkoa Singida Fenny Mashanjala akiongea kabla ya makabidhiano hayo yaliyofanyika katika ofisi ya kamanda wa Polisi mkoani hapa.

Wadau mbalimbali wakifuatiulia tukio hilo.

SSP Nestory Didi Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Mkoa Singida akitoa taarifa juu ya zoezi la ukaguzi linavyofanyika kuelekea siku kuu ya xmass na mwaka mpya.

SP Bakari kazungu kutoka wilaya ya Manyoni akiongea baada ya kukabidhiwa gari mpya kwaajiri ya ukaguzi wa usalama barabarani.

Katika kipindi cha miezi sita madeleva kumi wa mabasi wamefungiwa leseni zao na kusimamishwa kwa makosa mbalimbali ya barabarani mkoni singida. 

Hayo yamesemwa na Mkuu wa kikosi cha Usalama Barabarani Mkoani Singida SSP NESTORY DIDI wakati wa afra fupi ya kukabidhiwa Gari aina ya TOYAOTA PROBOX na  kamati ya Usalama barabarani gari hilo itatumika kwenye shughuri za usalama  Wilayani  Manyoni Mkoani hapa.

Naye makamu mwenyekiti wa usalama barabarani Fenny Mashanjala amesema kuwa gari lililotolewa litumike ipasavyo hasa katika sehemu zenye misongamano kama mlima Saranda na sehemu tete wakati wote ili kuepuka ajali.

Kamati hiyo ya usalama barabarani iliyoundwa Kwa mjibu wa kifungu Cha 96'99(c) Cha sheria ya usalama barabarani CAP 168 kama ilivyofanyiwa mapitio mara kwa mara.

Majukumu ya kamati hiyo ni pamoja na kufanya utafiti  mbalimbali juu ya sababu za ajali kutokea,kutoa ushauri kwa jinsi ya kuzuia ajali,kutambua maeneo tete na kulishauri jeshi la polisi,kutoa ushauri wa sheria za usalama barabarani zilizopitwa na wakati ili ziweze kufanyiwa marekebisho.

Kwa sasa hali ya usalama barabarani kwa mkoa huu  ni shwari kwa wilaya zote tano zilizopitiwa na barabara kuu (Highway) yani wilaya ya Singida, Manyoni,Ikungi,Mkalama,na Iramba.

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments