SERIKALI KUFANYA TAFITI NCHI.

 

Mkuu wa Mkoa Singida Peter Serukamba akitoa Taarifa hiyo kwa wanahabari Ofisini kwake Mjini Singida.

Naing'oya Kipuyo Meneja Takwimu Ofisi ya Taifa ya Takwimu Mkoa akitoa ufafanuzi juu ya Tafiti hizo.

Tanzania  inatekeleza tafiti tatu za kitakwimu ambazo zinafanyika katika mikoa yote nchini ukiwemo mkoa wa Singida.Tafiti hizo ni utafiti wa Shughuli za Kiuchumi na Kijamii Utafiti wa Kilimo wa Mwaka 2022/23 na Utafiti wa Kutathimini Upatikanaji Endelevu wa Huduma za Maji.

Kauli hiyo imetolewa na Meneja waTakwimu Ofisi ya Taifa ya Takwimu mkoa wa Singida Nain’ngoya Kipuyo wakati akitoa ufafanuzi juu ya Tafiti hizo.

Kipuyo amesema kuwa kwa upande wa Tafiti za Kiuchumi na Kijamii kwa Mwaka 2023/24 unausisha shuguhli za Ofisi zote zinazofanya kazi katika jengo au majengo ya kudumu nchini Tanzania.

Naye Mkuu wa Mkoa Singida Peter Serukamba ametoa wito kwa wananchi Mkoani hapa kutoa UShirikiano kwa wataalamu hao pindi watakapofika katika maeneo yenu.


Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments