Mtoto wa miaka sita asafiri peke yake Angani

 


Mtoto wa miaka sita alisafiri peke yake hadi mji mwingine nchini Marekani baada ya "kuwekwa kimakosa" kwenye ndege ya Shirika la Ndege la Spirit.

Casper alikuwa anasafiri kutoka Philadelphia kukutana na bibi yake mjini Fort Myers, Florida. Lakini aliishia Orlando - mwendo wa saa nne kwa gari kutoka Fort Myers - baada ya kuingizwa kimakosa kwenye ndege tofauti.

Shirika la ndege la Spirit limeomba msamaha na kujitolea kumlipa bibi yake gharama ya usafiri wa kwenda kumchukua Casper.

Casper alitarajiwa kusafiri kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Philadelphia hadi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Florida Kusini-magharibi huko Fort Myers siku ya Alhamisi, kukutana na bibi yake, Maria Ramos.

Lakini katika tukio linalozua kumbukubu ya filamu ya Home Alone 2, Kevin akapanda ndege isiyofaa - na kuishia kukwama mbali na familia yake wakati wa Krismasi, Casper alipandishwa kwenye ndege hadi Orlando, ambayo ni maili 160 (260km) kutoka Fort Myers.

Baada ya mtoto huyo kukosekana kwenye ndege aliyotakiwa kupanda, Bi Ramos aliingiwa na hofu.

"Nilikimbia na kuingia kwenye ndege hadi kwa mhudumu wa ndege na nikamuuliza, 'Mjukuu wangu yuko wapi? Alikabidhiwa kwako huko Philadelphia?''

Bi Ramos aliambia WINK-TV, kituo cha televisheni cha Fort Myers.

Alisema mhudumu wa ndege alimwambia: "Hapana, sikukabidhiwa mtoto."

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments