WAZEE WAELEZA CHANGAMOTO ZAO KWA SERIKALI


Katibu wa NEC Idara ya Organization Ngd Issa Gavu akiongea na Wazee wa Mkoa wa Singida katika ukumbi wa chuo cha VETA.


Katibu wa CCM Mkoa wa Singida Lucy Shee akiwakaribisha wajumbe wa mkutano huo.


Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida Mather Mlata akimkaribisha MNEC Issa Gavu kuongea na wazee wa mkoa wa Singida.



Wazee na Viongozi mbalimbali wa chama na Serikali wakimsikiliza MNEC  Ndg Issa Gavu Katika mkutano huo.




Kulia Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida na Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi  Betha Nakomolwa.


                                                    Makatibu kutoka Wilaya za Ikungi,Singida DC na Manyoni .


Wazee wa Mkoa wa Singida wameiomba serikali kujenga uwanja wa ndege mpya au kukarabati uliopo ili kurahisisha usafirishaji na kuongeza kasi ya maendeleo.

Wameyasema hayo katika kikao cha baraza la wazee Mkoa wa Singida na katibu wa NEC idara ya Oganaizesheni Ndg. Issa Gavu aliyefika mkoani hapo kwa lengo la kuzungumza na wazee na kusikiliza kero zao

Pamoja na kueleza changamoto mbalimbali wazee hao wameomba pia kuwekewa utaratibu mzuri wa kuhudumiwa wazee katika huduma za Afya na pia wastaafu kulipwa mafao yao kwa wakati.

Akijibu baadhi ya changamoto walizozisema wazee hao Mbunge wa jimbo la Singida mjini Musa Sima amesema serikali imeweka mikakati kwa ajili ya bima za afya kwa kila mtu na pia ujenzi wa viwanja vya ndege 13 nchini ukiwemo ukiwemo uwanja wa Singida.

Hata hivyo mgeni rasmi wa kikao hicho Ndg. Issa Gavu amesema kuwa uzee ni tunu na wazee ni watu muhimu katika kusimamia maadili na mienendo ya chama na hivyo chana na serikali vinatakiwa kuwaenzi wazee ili kusaidia kutekeleza ilani .


Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments