WANANCHI FANYENI MAANDALIZI YA KILIMO .


    Afisa Kilimo Wilaya ya Ikungi Gulisha Msemo amewataka wananchi kufika kwenye ofisi za watendaji kujiandikisha na kupata maelekezo na ufafanuzi juu ya Mbegu za Ruzuku.

                                 Madiwani wakifuatilia maelezo ya Agenda ya Kilimo.

 SINGIDA

10.11.2023

Viongozi Wametakiwa kuwahamasisha wananchi kufanya maandalizi ya kilimo mapema ili kufikia malengo wanayoyaweka ya kupata chakula cha kutosha na kujiinua kiuchumi.

Maagizo hayo yametolewa na mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Ally yote yatauzwa kwa mfumo wa ushirika wa stakabadhi ghalani.

Mwanga wakati akifungua kikao cha baraza la madiwani wilayani humo.

Mwanga amesema zaidi ya asilimia 75 wa halmashauri hiyo wanategemea kilimo hivyo ni vizuri wakafanya maandalizi mapema kwani baadhi ya maeneo mvua zimeanza kunyesha.

Katika hatua nyingine Mwanga amesema ratiba za usambazaji wa mbolea za ruzuku kwa kila kata zitolewe mapema ili wananchi waandae pesa na kusogea katika vituo ambavyo mbolea hizo zitagawiwa kwa wananchi kwa bei ya ruzuku.

Naye Afisa kilimo wa halmashauri hiyo Gulisha Msemo amesema wameweka utaratibu mzuri wa kuwasogezea wananchi mbolea ya ruzuku karibu na maeneo yao huku akiongeza mazao mengine 3 ya kibiashara na chakura.

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments