![]() |
Meya wa manispaa ya Musoma Mh Capten Mstaafu Wiliam Gumbo akiongea na Mtayalishaji wa kipindi cha Mtukio wa Standandard Fm 90.1 Singida Revocatus Phias maeneo ya Stend ya Misuna Singida mjini. |
Jumla ya madiwani 20 na wakuu wa Idara kumi kutoka katika halmashauri ya
manispaa ya Musoma wamefanya ziara ya kuitembelea halmashauri ya manispaa ya
Singida ilikuona jinsi manispaaa ya Singida inavyo tekeleza miradi mbalimbali
inayo fadhiliwa na benki ya Dunia.
Akiongea na standard redio Kepten Mtafu Wiliamu Patrick Gumbo ambaye ni
meya wa manispaa ya Musoma amesema nao ni miongoni mwa halmashari kumi na tano
inayotekeleza miradi inayofadhiliwa na benki hiyo.
Kapten Gumbo amesema katika vikao mbalimbali halmashauri ya manispaa ya
Singida inasifiwa kwa kutekeleza miradi hiyo kwa kiwango kinacho takiwa hali iliyowapa msukumo
wa kuja kujifunza jinsi wanavyo itekeleza.
Amesema wametembelea miradi ya barabara zinazo endelea kujengwa katikati
mwa mji huku wakitembelea stedi kuu ya mabasi ambayo amesema stendi hiyo ni miongoni
mwa stedi bora nchini.
Katika hatua nyingine Kapten Wiliamu amewaomba wananchi katika manispaa
ya Singida kujenga tabia ya kupisha miradi ya maendeleo kwani nifrusa katika
kukuza uchumi wao na taifa kwa ujumla.
0 Comments