Na,Jumbe Ismailly HANANG Feb,27,2018
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Hanang,Mkoani Manyara kimesema ifikapo mwaka 2020 wilaya hiyo haitakuwa na chama chochote kile cha upinzani kitakachoendelea kuwepo kutokana na serikali kushughulikia changamoto mbali mbali zilizokuwa kero kwa wananchi.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mwenezi wa CCM,Wilaya ya Hanang,Mkoani Manyara,Rogert Petro Toronto alipokuwa akitoa taarifa ya idadi ya wanachama waliohama kutoka katika vyama vya CHADEMA na CUF na kujiunga na CCM wakati wa ziara ya Mbunge wa jimbo la Hanang,Dk.Mary Nagu ya kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo pamoja na kuwashukuru wananchi kwa kumchagua kwa kura nyingi kuwa mbunge wa jimbo hilo.
Katibu mwenezi huyo aliweka bayana kwamba katika ziara ya Mbunge wa jimbo hilo pamoja na Mwenyekiti wa CCM wilaya hiyo waliyofanya katika kipindi cha kuanzia januari hadi sasa,walipokea jumla ya wanachama 274 akiwepo aliyekuwa mwenyekiti wa Kijiji cha Measkron aliyejiuzulu na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kujiunga na CCM.
Kwa mujibu wa katibu mwenezi huyo katika kata ya Gitanuwasi walipokea wanachama wapya 55 na 10 kutoka vyama vya upinzani,ambao kati yao watano walitoka CHADEMA na wengine watano walitoka CUF,wakati kata ya Measkroni wanachama 70 na kutoka katika vyama vya upinzani 8 walitoka CHADEMA.
Aidha Toronto alisema pia kwamba katika kata ya Balangdalalu jumuiya ya vijana wa CCM, (UVCCM) walipokea wanachama wapya 24 na kutoka BAWACHA wanachama 48 na katika kata ya Kateshi mjini wanachama wapya 55 na hivyo kufanya jumla ya wanachama wote waliojiunga na chama hicho kufikia 274.
Kwa mujibu wa katibu huyo wilaya ya Hanang ina jumla ya kata 33,ambazo kati ya hizo,kata 22 ni za CCM na wapinzani wana kata 11.Naye katibu wa CCM wilaya ya Hanang,Teddy Athumani aliyefika kwa mara ya kwanza katika Kijiji hicho aliweka bayana kuwa wamefuatana na Mwenyekiti wa wilaya kwa kazi moja tu ya kuwapokea wanachama wapya waliovihama vyama vya upinzani na kujiunga na chama hicho.
Akizungumza kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti wa CCM wilaya kupokea wanachama wapya,katibu mwenezi wa ccm wilaya,Rogert Petro Toronto aliwataka wanachama kuhakikisha wanachagua viongozi wote kutoka serikali ya CCM katika uchaguzi ujao wa serikali za mitaa.
Akipokea wanachama wapya waliohama kutoka vyama vya CHADEMA na CUF,Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Hanang,Methew Darema aliwahakikishia wananchi hao kwamba serikali ya awamu ya tano ni ya vitendo na siyo ya maneno matupu
Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Hanang,Mkoani Manyara,Rogert Peetro Torinto akiongea na wananchi wa Kijiji cha Diyagwa kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti wa CCM wilaya kupokea wanachama wapya.
mmoja wa wanakikundi cha kwaya katika Kijiji ch Diyagwa akimuonyesha Mbunge wa jimbo la Hanang,Dk.Mary Nagu maji wanayokunywa kutokana kutokuwa kukosekana kwa huduma ya maji safi na salama
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Hanang,Mkoani Manyara,Methew Darema akimkabidhi kadi ya CCM mmoja wa wanachama waliojiunga na chama hicho baada ya kuhama kutoka CHADEMA.
Mbunge wa jimbo la Hanang,Mkoani Manyara,DK.MARY NAGU akiwasalimia wananchi waliohudhuria mkutano huo uliolenga kuwapokea wanachama wapya wa chama hicho.(Picha zote Na Jumbe Ismailly)

0 Comments