Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida ACP Debora Magirigimba |
Wananchi
mkoani Singida wametakiwa kuacha kujichukulia hatua mikononi dhidi ya wahalifu
wanaokamatwa katika maeneo mbalimbali bali wawapeleke katika maeneo husika
ilisheria ichukue mkondo wake.
Kauli
hiyo imetolewa na kamanda wa jeshi la polis mkoani Singida Debora Magiligimba
wakati akiongea na standard redio ofisini kwake kuhusu suala usalama katika
mkoa.
Kamanda
Magiligimba amesema kwasasa hali ya mkoa imeimarika kiusalama kutokana na
ushiriki mkubwa wa wananchi kutoa taarifa kabala ya uhalifu na polis
kufuatailia hatimaye kudhibiti mapema.
Aidha
kamanda ameongea kuwa mbali nawananchi
kutoa ushirikiano mzuri limeibuka suala la wananchi kujichukulia sharia
mkononi suala ambalo amesema ni kinyume cha sharia.
Katika
hatua nyinge amesema jeshi la polis linataendelea kutoa elimu kwa wananchi
katika maeneo mbalimbali ilikungeza ushirikia na jeshi hilo huku akiongeza kuwa
ratiba yake ya kuzunguka katika nyumba za ibada kutoa elimu inaendelea.
0 Comments