KATAVI
Wanafunzi nchini
wametakiwa kusoma kwa bidii ili kutimiza ndoto zao na kuwa tegemeo kwa familia
zao pamoja na Taifa kwa ujumla, kufuatia juhudi za Serikali kuendelea kuwekeza
katika miundombinu ya elimu ya juu.
Wito huo umetolewa leo Machi 14, 2026 na Waziri Mkuu, Mwigulu Lameck Nchemba, wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa Jengo la Taaluma na Bweni la wanafunzi katika Kampasi ya Mizengo Pinda ya Sokoine University of Agriculture iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe mkoani Katavi Region.
Mradi huo wenye thamani
ya shilingi bilioni 17.4 unahusisha ujenzi wa jengo la taaluma litakalokuwa na
kumbi za mihadhara pamoja na maabara mbalimbali kwa ajili ya kujifunzia, ambapo
linatarajiwa kuhudumia takribani wanafunzi 2,000 kwa wakati mmoja. Aidha,
kutajengwa bweni la kisasa litakalokuwa na uwezo wa kulaza wanafunzi 400.
Akizungumza katika
hafla hiyo, Dkt. Nchemba amesema mradi huo ni sehemu ya utekelezaji wa maono ya
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ya kuimarisha
taasisi za elimu ya juu ili kuongeza fursa za vijana kupata elimu bora nchini.
Katika hatua nyingine,
Waziri Mkuu aliwataka wananchi kuendelea kumuombea aliyekuwa Waziri Mkuu
Mstaafu, Mizengo Pinda, ambaye kampasi hiyo imepewa jina lake kwa kutambua
mchango wake mkubwa katika maendeleo ya elimu na uongozi nchini.






0 Comments