Rais wa Shirikisho la wachimbaji madini wadogo nchini FEMATA akiongea katika kikao cha Sekretariet .

Kamisha wa madini Terence Ngole akiongea na wajumbe wa sekretariet katika kikao maalum kilochofanyika jijini Dodoma.
DODOMA
Shirikisho la Wachimbaji Wadogo wa Madini Nchini (FEMATA)
limefanya kikao chake cha kwanza cha sekretarieti baada ya Uchaguzi Mkuu wa
Awamu ya Sita, kikao kilichofanyika jijini Dodoma katika ukumbi wa African
Dreams Hotel.
Kikao hicho kimeongozwa na Rais wa FEMATA, John Bina,
sambamba na Makamu Rais Victor Tesha, na Katibu Mkuu Elies Rodgers. Washiriki
walikuwa ni wajumbe wa kamati mbalimbali za shirikisho hilo pamoja na viongozi
wa wachimbaji wadogo kutoka mikoa yote nchini.
Mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Eng.
Yahaya Samamba, aliyewakilishwa na Kaimu Kamishna wa Madini, Terence Ngole.
Katika kikao hicho, FEMATA imeipongeza Serikali kupitia Wizara ya Madini chini ya uongozi wa Waziri Anthony Mavunde na Naibu Waziri wake, kwa jitihada mbalimbali za kuboresha sekta ya madini na kuweka mazingira rafiki kwa wachimbaji wadogo.
Sekretarieti imejadili kwa kina mustakabali wa sekta ya
uchimbaji mdogo na kupitisha maazimio saba ,Femata itayakabidhi maazimio hayo
kwa Waziri wa Madini mwezi Januari.
1-Kuondoa
migongano ya kimasilahi katika shughuli za uchimbaji na kuboresha mifumo ya
utatuzi wa migogoro.
2-Kuandaa mpango
kazi wa FEMATA utakaowasilishwa rasmi serikalini kwa utekelezaji.
3-Kuthibitisha
msimamo kuwa FEMATA si chama cha kiarakati, bali ni chombo cha majadiliano na
ushirikiano wa kiserikali.
4-Kuimarisha
mahusiano kati ya wachimbaji wadogo na makamishna wa madini katika mikoa.
5-Kuunda na
kuimarisha Kamati ya Maadili itayosimamia nidhamu na matumizi sahihi ya
mitandao ya kijamii.
6-Kuomba serikali
iendelee kuwajengea uwezo wachimbaji wadogo ili kuongeza tija na usalama
migodini.
7-Kutafuta
ufumbuzi wa changamoto ya nishati migodini, ikiwemo upatikanaji wa umeme na
mafuta kwa gharama nafuu.
FEMATA pia imeomba serikali kuharakisha mpango wa kuitangaza
Tanzania kama kitovu cha biashara ya madini Afrika, kwa kuweka mazingira bora
zaidi kwa wauzaji, wanunuzi na wawekezaji.
Kwa mujibu wa takwimu, zaidi ya asilimia 70 ya vijana nchini wanajihusisha na shughuli za uchimbaji madini, huku FEMATA ikiwa na wanachama wanaokadiriwa kufikia milioni 6.









0 Comments