Mwenyekiti wa Supatanza Mkoa wa Singidsa akiongea na mwandishi wetu mjini Singida.
Singida
Mwenyekiti wa SUPATANZA Mkoa wa Singida na mchezajiwa zamani wa Singida United na
Mtibwa Sukari na mwalimu wa Singida Veteran Edwin Agai amesema kuwa baadi ya
migogolo baina ya timu za likuu bara inasababishwa na waalimu kujalibu kuiga
tama duni za mashariki ya mbali ya kuwakataa wachezaji waliyo sajiriwa na
uongozi bila kujua kuwa tayari mchezaji huyo ameshaingia makubaliano na timu
husika.
Akiongea na Radio kicheko live mjini
Singida Agai amesema kuwa viongozi wa timu wanatakiwa kufuata makubaliano
yaliyofikiwa baina ya timu na mchezaji huku akitolea mfano timu ya Dodoma jiji.
Akizungumzia uongozi mpya wa timu ya
Singida Veteran uliyochaguliwa hivi karibuni agai amesema kuwa amefarijika
kutokana na utekelezwaji wa ununuzi wa Vifaa vilivyokuwa vinakosekana katika
timu hiyo sambamba na kutoshiriki mashindano ya Veteran yanayotajwa kufanyika
hivi karibuni.
0 Comments