TAHA ni Asasi ya kilele ya sekta binafsi yenye lengo kuu la kuhamasisha maendeleo ya mazao ya kilimo cha mboga mboga (horticulture) hapa nchini imekamilisha uchimbaji wa kisima cha maji kwaajili ya shughuli za kilimo cha umwagiliaji Wilayani Ikungi.
Akizungumza na vikundi vilivyo fika kwenye uzinduzi wa uwekwaji wa pampu kwenye kisima mkuu wa Wilay ya ikungi Edward Mpogolo amesema kuwa kuwepo kwa kisima hicho kitawawezesha Wanawake wanaoendesha kilimo hicho kufanya shughuli zao kwa ufanisi zaidi.
"Hakika Taha mmewakomboa wanawake kwa kuwaletea shamba darasa na kuwachimbia kisima ili kuwanyanyua kiuchumi watu wa Ikungi kwa kulima mboga mboga matunda, viungo na mazao ya mizizi. kutoka maeneo ya vijiji vya Munyu,Mnan'gana na Kipumbwiko wilayani Ikungi"
Mpogolo aliongeza kuwa watu wote waliopo kwenye huu mradi wahakikishe wanafanya kazi kwa bidii ili waweze kupata mafanikio na kutunza miundombinu yote itakayo wekwa kwenye mashamba yote mradi unapo fanyakazi na kama nikisikia kuna mtu au watu watafanya uhujumu basi hatasita kuwachukulia hatua kali za kisheria, kwani Serikali imeweka nguvu kubwa kwenye eneo hili kupitia TAHA kwahiyo wafanye kazi kwa bidii na kuheshimiana.
Asasi hiyo kwa kushirikiana na UN WOMEN na KOICA kwa pamoja wemekamilisha uchimbaji wa kisima kimoja cha maji katika Kata ya Kipumbwiko wilayani Ikungi mkoani hapa ili kuimarisha na kuleta tija kwa wakulima wa zao hilo.
Mradi huo utatekelezwa kwa miaka 3 kwa ufadhili wa Shirika la UN Women huku TAHA kwa kushirikiana na Shirika hilo,KOICA pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi lengo likiwa ni kuwakomboa wanawake kiuchumi.
mradi huo umejikita zaidi kuwawezesha wanawake katika mnyororo wa thamani wa mazao ya mboga mboga, matunda, viungo na mazao ya mizizi.
Awali Akitoa
Taarifa ya mradi kwa mkuu wa Wilaya ya Ikungi meneja wa mradi kutoka TAHA
Elianche Shang'a
alisema visima vya mradi huo ambavyo vinachimbwa na Kampuni ya Ahia General Supplies, kuwa kisima hicho chenye urefu wa mita 100 kwenda chini kimekamilika.
Aliongeza kwa kusema kuwa maji yanayopatikana katika kisima hichi ni kuanzia lita 5,000 kwa saa, hivyo basi kuna uhakika wa kuendesha kilimo cha mboga mboga bila shaka yoyote.
"Kisima hiki kimechimbwa kwa ubora wa hali ya juu kimekamilika na leo. Utashudia uwekwaji wa pampu, kinauwezo wa kudumu zaidi ya miaka 100 hivyo wanakikundi watarajie mafanikio makubwa kwani maji yanayotoka hapa ni yakutosha kwa masaa 24." alisema Shang'a.
Kwa upande wa wanufaika wa mradi huo Katibu wa Kikundi cha chapakazi Elizaberth Salum- kinacholima Mboga-mboga kwenye shamba la Kikundi alisema matarajio yao ni kutumia shamba darasa hilo kwenda kuboresha shughuli zao za Kilimo cha Mboga Mboga ili kuongeza kipato kitakachosaidia katika kujikomboa kiuchumi.
TAHA inaendesha kazi zake katika mikoa 25 ya Tanzania ikiwemo Arusha, Mwanza, Manyara, Kilimanjaro,Tanga, Dodoma, Morogoro, Iringa, Njombe, Pwani, Dar es salaam, Lindi, Mtwara, Mara, Simiyu, Mbeya, Songwe.
Unguja (Unguja Kaskazini, Unguja Kusini na mjini Magharibi ),Pemba ( Pemba Kaskazini na Pemba Kusini ), Ikungi-Singida pamoja na Msalala-Shinyanga.
Wadau wanaowezeshwa katika mnyororo huo wa thamani ni wasambazaji wa pembejeo, wakulima, wasindikaji, wafanyabiashara, wasafirishaji na makampuni yanayofanya usafirishaji nje ya nchi na wanawawezesha kwa vitendo.
Kazi kubwa zinazofanywa na TAHA ni kuwaunganisha wakulima na masoko,kuwawezesha wakulima katika suala zima la kilimo na kuwaonesha teknolojia mbalimbali ambazo wanaweza kuzitumia kulingana na uwezo na mazingira waliopo
kutengeneza
mazingira wezeshi ya biashara na kufanya kazi hiyo kwa kushirikiana kwa karibu
na serikali kuu kwa maana ya kushawishi na kutetea mzalishaji,mfanyabiasha na
mdau yeyote katika mnyororo wa thamani,kuwaunganisha wadau katika mnyororo wa
thamani na vyombo vya fedha baada ya kuwafundisha elimu ya fedha.







0 Comments