MWONEKANO WA NGULI WA SOKA BARANI AFRIKA WAZUA GUMZO MITANDAONI



Mchezaji wa zamani wa Ivory Coast na Chelsea Didier Drogba amesema watu hawafai kushangazwa sana na hatua yake kunyoa nywele ingawa amekiri maisha yake yameimarika.
Aidha amezungumzia uchezaji wa klabu za Afrika katika Kombe la Dunia.
Kuhusu hatua yake kukata nywele zake, amesema hilo halikuwa jambo la ajabu sana kwake.
"Ni jambo nililokuwa nimelifanya miezi kama saba hivi iliyopita, lakini nafikiri mimi si mzuri sana katika kuweka mambo mitandao ya kijamii - huwe siwezi selfie za kutosha," amesema.
"Kwa hivyo, ninajua ni jambo watu wengi hawajalizoea, kwa sababu nilikuwa na nywele ndefu kwa miaka mingi - lakini kuwa bila nywele ndefu si jambo geni."
Amesema hata hivyo kwamba "huwa inarahisisha mambo."
"Kwa sababu sasa huwa situmii muda mwingi kwenye bafu," amesema Drogba akihojiwa na BBC.
VIPI KUHUSU TIMU ZA AFRIKA URUSI
Mataifa ya Afrika hayajapata matokeo ya kuridhisha Kombe la Dunia isipokuwa Senegal na Nigeria ambao wameshinda mechi moja kila mmoja.
Misri na Morocco tayari zimeyaaga mashindano na matumaini ni finyu kwa Tunisia baada yao kushindwa 5-2 na Ubelgiji mechi yao ya pili.
Drogba anasema Nigeria, mechi yao dhidi ya Iceland, walicheza jinsia anavyotaka kuona nchi za Afrika zikicheza "kwa kushambulia, kutumia kasi na nguvu, na kushambulia goli mara nyingi."
Anasema hilo halikuwepo walipochapwa na Croatia mechi yao ya kwanza.
"Walikuwa wanacheza wenyewe - kujiweka sawa, kujilinda bila kushambulia, na kwa kutoa pasi sehemu moja ya uwanja hadi nyingine," amesema.
"Wakati huu (dhidi ya Iceland) walicheza kushinda. Walikuwa na washambuliaji wawili na walikuwa na kasi sana na ukali wakishambulia kiasi kwamba Iceland waliingiwa na asiwasi.
Walikuwa hawatabiriki kwa mashambulizi na walivutia sana.
"Nilitarajia wacheze hivi Kombe la Dunia - na ndio maana wakashinda mechi hiyo," anasema.
Anaongeza kuwa mataifa ya Afrika yakicheza Kombe la Dunia yanafaa kudumisha utambulisho wao kama time, na anasema ni Senegal pekee waliokuwa wamefanikiwa kufanya hivyo kabla ya Nigeria mechi yao ya pili.
"Ni muhimu kwao kuendelea kufanya hivyo - na Nigeria pia - ili wafike hatua ya 16 bora. Wakiamua kucheza mchezo wa kujilinda na kuanza kuogopa kufungwa, watarudi nyumbani."

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments