Mtu mmoja ameelezwa kuwa ''mtalii
mjinga ambaye hajapata kutokea'' baada ya kutoa mkono wake na kumpapasa Simba
Tanzania.
Picha za video za tukio hilo la ajabu zilionyesha mwanaume huyo
akipapasa manyoya ya simba huku akipiga picha kwa kutumia simu yake ya mkononi
katika hifadhi ya taifa ya Serengeti nchini Tanzania.
Simba aligeuka haraka akatazama dirisha lililo wazi, kisha
akanguruma ishara kuwa yuko tayari kushambulia, watalii waliokuwa ndani ya gari
waliruka na kuharakisha kufunga kioo baada ya sauti iliyosikika ikipayuka
''funga kioo''
Picha hizo zilitolewa kwenye mtandao wa Youtube ukiwa na jina
''Watalii wajinga kupata kutokea'' Watu wengi wakikosoa
kilichofanywa na watalii hao.
Inaaminika kuwa simba ambaye awali alionekana kwenye video
alikuwa karibu na gari ya watalii akitafuta kivuli.
Katika Video hiyo iliandikwa: ''Simba mara kadhaa hutumia magari
kupata kivuli kama eneo halina miti, lakini haina maana kuwa simba wanawaamini
binaadamu''.
''Kujaribu kuwashika ni jambo la kijinga sana lililofanywa na watalii
hao''.
Mlinzi wa mbuga nchini Afrika Kusini Naas Smit aliliambia jarida
la The Sun kuwa ''Wanaofanya kazi kwenye mbuga wanafahamu kasi ya simba na
angeweza kujeruhi mkono wa mtu aliyemgusa.
''angekuwa na nguvu za kuwavuta watalii kupitia kwenye dirisha
na kuwaua papo hapo mbele ya marafiki zao lilikuwa jambo la kijinga sana
kufanya''.
''Ilikuwa bahati sana walinusurika simba ni wanyama hatari
sana''
''Kama simba angemuua mtu kwenye eneo hilo askari wangepaswa
kumuua simba hasa kama angakuwa dume, vinginevyo kungekuwa na madhara
makubwa," alieleza Smit.
0 Comments