Bw Nehemia Msechu aliyekuwa mkurugenzi wa shirika la nyumba nchini (NHC) |
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi
ametengua uteuzi wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)
Nehemia Mchechu.
Kupitia Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi,
Dorothy Mwanyika imesema kuwa kwa mamlaka aliyonayo waziri Lukuvi chini ya
kifungu cha 18(1) cha sheria ya Shirika la Nyumba la taifa amesitisha uteuzi
huo kuanzia leo Juni 20, 2018.
“Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi
kwa mamlaka aliyonayo chini ya kifungu cha 18(I) cha sheria ya Shirika la
Nyumba la Taifa ya mwaka 1990 pamoja na marekebisho yake mwaka 2005, ametengua
uteuzi wa mkurugenzi wa shirika hilo”, imesema Taarifa.
Awali katika taarifa iliyotolewa na Msemaji Mkuu wa Serikali
Dkt. Hassan Abbasi Disemba 16, 2017 ilimtaka mkurugenzi huyo kusimama majukumu
yake ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zilizokuwa zikimkabiri za utendaji mbovu.
0 Comments