Na Thomas kiani.
Singida.
KIJANA mmoja mkazi wa kijiji cha Musimi kata ya Sepuka Wilaya ya
Ikungi Mkoa wa Singida Ali Ali Juma (32) ameuawa kikatili na watu
wasiofahamika kwa kukatwa sehemu mbalimbali za mwili wake akatobolewa macho na
kuvuliwa nguo zote juzi usiku.
Akizungumza na mwandishi wa habari jana katika kijiji
hicho kaka yake mkubwa Hamadi Ali Juma amesema tukio hilo la kuuawa kwa mdogo
wake kikatili na watu wasiofahamika limemsikitisha sana na ndugu wote
baada ya kupata taarifa kwamba kuna mtu ameuawa Sepuka Madukani kwenye Hifadhi,
njia ya kwenda Shuleni Musimi.
Hamadi amesema alipata habari za uhakika kutoka kwa mkwe wake
aitwae Hamisi kwamba ni Ali ambae ni mdogo wake wa mwisho kutoka kuzaliwa kwa
Baba yao na kabla hajaondoka ikaja pikipiki kumchukua hapo hapo akawa ametambua
kilichoendelea.
Ameendelea kusema alipofika kitu cha kwanza aliangalia nguo zake
akazifahamu zikiwa mbali mita moja kutoka mwili wa marehemu na alipomsogelea
hakuweza kumfahamu haraka lakini baadae akamfahamu akiwa ametapakaa damu kichwa
chote, macho hakuna na mwili wote ukiwa na majeraha na damu.
Hamadi amesema mdogo wake amekufa kifo kibaya ameuawa kikatili
sana alitobolewa macho, shingo na kisoga upande wa kushoto ilikatwa na kitu
chenye ncha kali, uso na sikio upande wa kulia amekatwa, bega la kulia
lilikatwa, mikono yote ilikatwa na miguu yake ilikuwa na majeraha ya kukatwa
huku nguo zake zimewekwa pembeni.
Aidha Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Musimi Ramadhani Mlali
amesema alipata taarifa hizo asubuhi kwa Simu akiwa ofisini kwake kwamba katika
hifadhi ya kijiji wanafunzi wa Shule za msingi ambao wako kambini Umitashumta
Musimi wamemuona mtu mmoja amekufa njiani.
Mlali amesema alipofika hakuweza kumfahamu haraka kwa vile
alishaanza kuvimba alikua hana nguo akaomba msaada wa Nguo kwa msamaria mwema
akamfunika lakini baadae akamfahamu kwa jina la Ali.
Mwenyekiti wa kijiji cha Musimi Abubakari Mkanga amewataja watu
hao kuwa ni Hawa Rajabu, Asia Laizer, Mama Hashimu Mwantui Simioni Sungi na
Kisuda Nyoha na polisi bado wanaendelea na upelelezi ili kubaini
timu nzima iliyofanya vitendo hivyo vya kikatili.
Polisi walipofika walikua na Mganga Mfawidhi wa kituo cha Afya
Sepuka Dr. Charles Mngazija waliofanya uchunguzi na kubaini Majeraha
kadhaa makubwa ya kukatwa na kitu chenye ncha kali katika mwili wa marehemu Ali
na ndio yalisababisha kifo chake na baada ya uchunguzi huo ndugu waliruhusiwa
kuchukua mwili wa marehemu kwa maziko.
Kamanda wa Polisi Mkoani Singida Kamishina Msaidizi wa Polisi ACP
Debora Magilingimba amethibitisha kuwepo kwa tukio katika kijiji hicho kuwa
kijana huyo ameuawa na watu wasiofahamika juzi usiku hata hivyo Polisi
inawashikilia watu watano wakazi wa kijiji hicho kwa uchunguzi zaidi.
0 Comments