![]() |
Baada ya Yanga ya Dar Tz kuangukia katika mashindano ya Kombe la
Shirikisho Jumamosi ya jana, Yanga inaweza ikapangiwa kucheza na vigogo kadhaa
barani Afrika.
Bado haijapangwa kuwa Yanga itacheza na nani, ingawa timu
zilizopo kwenye mashindano hayo mojawapo ni Enyimba FC kutoka Nigeria.
Si Enyimba pekee, baadhi ya timu zingine zinazoshiriki Kombe la
Shirikisho ni Zamalek, Raja Cassablanca, SuperSport United ya Afrika Kusini na
Al Masry ya Misri.
Vigogo Enyimba leo watakuwa na kibarua kucheza dhidi ya Energie
FC. Katika mechi ya kwanza Enyimba alishinda jumla ya mabao 2-0.




0 Comments