WASICHANA 100 MATEKA WAACHIWA NIGERIA


Wasichana hao walitekwa katika shule hii ya Bweni Dapchi  jimbo la Yobo mwezi Februari mwak huu
Serikali ya Nigeria imesema wengi wa watoto 110 waliotekwa na wapiganaji wa Kiislami kutoka mji wa Dapchi mwezi uliopita wamerejeshwa.
Wizara ya habari nchini Nigeria imesema wanafunzi 101 kati ya 110 walirudishwa mapema hii leo baada ya 'juhudi za kichinichini za hapo awali.''

Jeshi ''lilisimamisha kwa muda'' operesheni katika eneo hilo ili kuhakikisha ''maisha ya watoto hao hayamo hatarini,'' taarifa hiyo imeendelea kusema.
Hata hivyo, taarifa hiyo haikuzingatia idadi ya wasichana waliofariki na imesema hakuna kikombozi kilicholipwa kwa wapiganaji hao.

Taarifa hata hivyo zinadokeza kwamba wasichana takriban watano walifariki wakiwa mateka, na msichana mmoja ambaye ni Mkristo bado hajasalimishwa na anaendelea kushikiliwa mateka.

Babake msichana huyo amesema anaendelea kuzuiliwa na wanamgambo hao kwa sababu amekataa kuslimu. Kwenye mahojiano na kituo kimoja cha redio, amesema ana furaha kwamba msichana huyo hakuikana dini yake.
Waziri wa habari na tamaduni, Alhaji Lai Mohammed, amesema kwenye taarifa kwamba wasichana hao waliachiliwa ''katika hali isiyo ya kawaida'' na kwa "usaidizi wa marafiki wa nchi hii.''

"Serikali ilikuwa na uhakika kwamba vita na majibizano havingekuwa suluhu kwani ingehatarisha zaidi maisha ya wasichana hao, na mfumo wa kutotumia nguvu ndio uliokuwa umependekezwa," Bw Mohammed aliongeza.


Pia alidokeza kwamba idadi hiyo huenda ikaongezeka kwa sababu wasichana hao hawakukabidhiwa kwa mtu binafsi , ili kutoa idadi rasmi ya wasichana hao.

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments