SINGIDA
Wananchi wametakiwa kuhakikisha wanaungana pamoja ilikupinga
suala zima la ukeketaji ambaolo ni ukatili wa kijinsia ilikuweza kuunga mkono
harakati za kupinga ukatili huo.
Rai hiyo imetolewa ma mwanasheria wa halimashauri ya wilaya
ya Singida Bi, Fotunata Matinde wakati
akiongea katika maadhimsho ya wiki ya
siku 16 za ukatili wa mwanamke na watoto maadhisho yaliyofanyika katika kata ya mtinko wilaya ya singida chini ya uratibu wa shirika la actionaid .
Bi, Fotunata amesema ukatili
wa kijinsia unapingwa kila mahali kote duniani kulingana na mikataba ya
kimataifa hukua akiwaomba wanachi kujitokeza ilikulipoti masuala hayo.
Amesema kulingana na elimu inayoendelea kutolewa kuhusiana
na masuala haya ya ukatili jamii inatakiwa kuamka na kutoa taarifa za ukatili
katika maeneo yao.
Kwaupande wake mwenyekiti wa jumuia ya wanawake Singida
Vijijini (SAPAWA) Bi, Amina Daffi amesema wanaendelea kupambana kwa toa elimu
mbalimbali kwa akina mama ilikuzitambua haki zao
0 Comments