Meneja ofisi ya Chamwino Dodoma na Singida Actionaid Bw Elias Mtinda akifafanua jambo juu ya siku ya mtoto wa Afrika. |
Mgeni Rasimi Mh Diwania wa kata ya Msisi Emmanuel Sima akifunga kikao hicho baada ya kujadili changamoto mbalimbali juu ya mtoto wa Afrika. |
Bw Kilonzo ni mratibu kutoka ACTIONAID akiongea na wadau wa Elimu waliyofika katika kikao hicho. |
Wanahabari wakifuatilia kwa makini mjadala unavyoendelea. |
Shirika la Action AID kwa kushirikiana na shirika la MEDO
ambao ni wadau wa elimu wamefanya
mkutano wa wadau wa elimu lengo likiwa ni kujadili changamototo zilizopo katika
sekta ya elimu katika kuelekea maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika .
Akizungumza baada ya mkutano huo manager wa shirika la
ACTION AID mkoa wa Singida Bw.Elias
Mtinda amsema kuwa mkutano huo
umefanyika katika kata ta Ilongero mkoani Singida ukiwa na dhumuni la kujadili
changamoto mbalimbali zinazoikumba sekta ya elimu ikiwa ni pamoja na
miundombinu.
Kwa upande wake mgeni rasmi katika mkutano huo ambaye ni
diwani wa kata ya Msisi Bw.Emmanuel Siima ametoa shukrani zake kwa muhisani
anaeandaa huduma ya maji katika shule mbalimbali katika kata hiyo.
Bw.Hussein Sharari ni afisa taaluma idara ya elimu msingi
amesema kuwa wana jumla ya walimu 836 ambapo amesema kuwa bado kuna upungufu wa
zaidi ya walimu 700.
0 Comments