SINGIDA United F.C. kupitia ligi ya mtoano ya Sport Pesa
Super Clup iliyomalizika hivi karibuni,imeonyesha ni bora zaidi ikilingnishwa
na timu ya Yanga na Simba.
Singida United pamoja na uchanga wake,iliweza kufunga goli dhidi
ya timu kongwe ya Kenya (Leopard) katika muda wa kawaida wa dakika 90.
Lakini timu hizo zenye umri mkubwa (Yanga na Simba)
kwenye ligi hiyo iliyofanyika kwenye uwanja wao wa nyumbani,zilisubiri
hadi hatua za kupigiana mikwaju ya penalty,ndipo zilipofanikiwa kufunga magoli.
Mdau wa Singida United na Mbunge wa jimbo la Iramba,Mwigulu
Nchemba,ametoa ‘kijembe’ hicho juzi kwa nyakati tofauti kwenye mikutano ya
hadhara iliyofanyika jimboni kwake.
Alisema Singida United ilifanya mazoezi kwa siku sita tu kwa
ajili ya ligi hiyo,imeonyesha ni timu yenye ushindani mkubwa.Hivyo timu
zitakazoshiriki ligi kuu msimu ujao,zitarajie vipingo,na si vinginevyo.
Mwigulu ambaye pia ni waziri wa mambo ya ndani,alisema
wanaendelea kutekeleza programu ya kukusanya vijana mkoani hapa wenye
vipaji vya mpira wa miguu.Watakaochaguliwa,vipaji vyao vitakuzwa,ili waje
kuitumikia timu yao ya nyumbani.
Katika hatua nyingine,katibu mkuu wa Singida United,Abdulrahaman
Sima,amesema Singida United inatarajia kuanza kambi ya mazoezi jijini
Dar-es-salaam au Mwanza, Julai mosi mwaka huu.
“Tunatamani sana mazoezi tungeyafanyia nyumbani Singida,lakini
kwa sasa hatuna kiwanja.Uwanja wa namfua bado upo kwenye ukarabati,hivyo
tunalazimika kutafuta uwanja nje ya mkoa wa Singida.
Hata hivyo,alisema watafanya juhudi za kuhakikisha Singida
United inacheza mechi ya kirafika mjini Singida kabla ya kuanza ligi kuu,ili
kuitambulisha kwa wapenzi wa soka na wananchi kwa ujumla.
0 Comments