Wakati bado ulimwengu wa michezo ukijadiliana namna Singida
United Fc ilivyowanasa wazimbabwe Muroiwa na Kutinyu walioongoza kikosi cha
timu yao ya Taifa pale Gabon kwenye michuano ya AFCON 2017.
Hii leo kupitia chanzo chetu cha uhakika mjini NAIROBI kenya
zinasema, Singida United Fc jana usiku walifanikiwa kuinasa saini ya beki
kisiki wa timu ya Taifa ya UGANDA ambaye aliongoza safu ya ulinzi ya timu ya
Taifa ya Uganda kwenye michuano ya AFCON 2017 pale Gabon.
Mmoja ya wajumbe wa kamati ya usajili ya Singida United Fc
ndg. Festo Sanga ametua jana Nairobi kumalizana na mchezaji huyo SHAFIK
BATAMBUZE (23) anayekipiga TUSKER FC ya Kenya.
Shafik msimu uliopita alikuwa ni mchezaji bora wa ligi ya kenya
kwa kuipatia ubingwa Tusker wa FA CUP na Premier League.
Kwa usajili huu, Singida United wameshafisha wachezaji
wakimataifa 4 ambao wote wapo kwenye timu zao za Taifa,watatu ni kutoka
zimbabwe(Elisha Muroiwa, Wisdom Mtasa na Twafaza Kutinyu) na sasa Mganda Shafik
Batambuze.
Picha ni Shafik Batambuze alikubali kandarasi ya miaka miwili
kuitumikia Singida United Fc, hapa akiitumikia timu yake ya Tasker Fc .
0 Comments