Klabu ya soka ya Singida United ambayo,
imepanda ligi kuu soka Tanzania bara na hivyo kutarajia kushiriki kwa mara ya
kwanza katika msimu mpya wa ligi, imepata msaada kutoka Benki ya NMB, ya vifaa
vya michezo vyenye thamani ya sh. milioni 10 .
Akizungumza
wakati wa kukabidhi msaada huo katika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es
Salaam, Ofisa Mkuu wa Wateja Wakubwa na Serikali, Richard Makungwa alisema
msaada huo umelenga kuisaidia timu hiyo kwa ajili ya kujiandaa kwa ligi.
“Tumetoa msaada huu kwa timu ya Singida United kwa ajili ya maandalizi
ya ligi hiyo na hii ni kawaida yetu kusaidia timu mbalimbali pale tunapopata
nafasi” alisema Makungwa.
Makungwa alisema,
licha ya benki hiyo kufanya shughuli za kibenki pia imejikita kuinua michezo
nchini kwa kutoa msaada wa vifaa vya michezo.
Katibu wa timu hiyo Abdurahman Sima alisema vifaa hivyo walivyopata
vitatumika kwa lengo lililokusudiwa na si vinginevyo.
“Tunaishukuru benki ya NMB kwa msaada huu
tunaomba wadau wengine kuiga mfano wa benki hii ” alisema Sima.
0 Comments