Kiungo wa kati wa Cameroon Christian
Bassogog, amejiunga na klabu ya China ya Henan Jianye, inayoshiriki michuano ya
ligi kuu ya Uchina kutoka klabu ya Aab Fodbold.
Mapema mwezi huu shambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 21
alitajwa kuwa mchezaji bora wa Afcom baada ya Cameroon kupata ushindi wao wa
tano kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika ya kombe la Taifa nchini
Gabon.
Aab imemuuza Bassogog kwa klabu ya Henan Jianye FC kwa rekodi ya
uhamisho kuelekea Aab, klabu hiyo imesema katika taarifa yake.
Bassogog amesema pendekezo la China hangeweza kulikataa.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Cameroon alishiriki mechi zote
sita katika Kombe la Mataifa , na kufunga bao katika hatua ya nusu fainali pale
Indomitable Lions walipowachapa Ghana 2-0.
Kwa sasa anakuwa miongoni mwa wachezaji wa kiafrika kuelekea
Uchina , baada ya mchezaji wa Nigeria John Mikel Obi na Odion Ighalo
walipojiunga na Tiajin Teda na Changchun Yatai mtawalia mwezi uliopita.
0 Comments