Waziri
wa Nchi Ofisi ya waziri Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira
na Walemavu Bi Jenista Mhagama amewataka wazazi kuzungumza na vijana wao kwa lengo
kuwasaidia namna ya kuepuka mimba katika umri mdogo
Waziri
Mhagama amesema hayo leo mchana katika uzinduzi wa kampeni ya kijana jitambue
wakati ni sasa iliyozinduliwa kwenye ukumbi wa mikutano RC mjini Singida
Amesema
akina mama hutumia muda mwingi katika shuguli za uzalishaji mali hali
inayopelekea watoto wao kuharibika kutokana na kutopata elimu sahihi kwa wakati
za sahihi juu ya mabadiliko ya miili yao
Amewataka
wazazi kuvaa ujasili kwa kuwaeleza ukweli vijana wao kuhusiana na kile
kinachoendelea
Amewakumbusha
wazazi kuwapa misimamo ya dini ili kuwa na hofu ya mungu hatua itakayosaidia
kukuwa katika misingi ya Imani.
0 Comments