Rais Obama wa ameamuru kutimuliwa kwa
wanadiplomaisa thelathini na tano wa Urusi kufuatia tuhuma za Urusi kutaka
kuingilia kati uchaguzi wa Marekani kupitia njia ya mtandao.
Makazi ya wanadiplomasia wawili wa Urusi yamefungwa na baadae
kuwekewa vikwazo.
Rais Obama amesema Urusi imekuwa ikiwadhalilisha maafisa wa
Marekani na ametahadharisha hatua zaidi kuchukuliwa.
Obama ameendelea kusema wamarekani wote sharti washtushwe na
vitendo vya Urusi, hii ikionekana kama njia ya kumjibu mrithi wake Donald Trump
ambae amesema kila mtu aishi maisha yake.
Kwa upande wake, rais mteule mara kwa mara amekuwa akizipuuzia
taarifa hizo za udukuzi, lakini hivi amesema atakutana na wakuu wa mashushu wa
Marekani ili kulijadili hilo.
Urusi nayo imekana tuhuma za kufanya udukuzi mfumo wa mtandao wa
chama cha Democratic.
Msemaji wa serikali ya Urusi amesema Urusi nayo italipiza kwa
kiwango hicho hicho.
0 Comments