Kaimu mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya ya singida Elias Jonh Tarimo akianagalia gwalide la mgambo |
Wahitimu
120 waliohitimu mafunzo ya mgambo katika
wilaya ya Singida wametakiwa kwenda kuyatumia mafunzo waliyoyapata kwa ajili ya
kuisaidia jamii hususani katika suala la ulinzi na usalama.
Hayo
yamesemwa na mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Singida
ambaye ni mkuu wa wilaya Ellias John Tarimo wakati akizungumza na wahitimu hao
na wananchi kwa ujumla kwenye hafla ya kufunga mafunzo hayo.
Tarimo
amesema kuwa mafunzo waliyoyapata wahitimu ni kielelezo tosha kinachowapambanua
kama askari walioiva kukabiliana na matukio ya kihalifu hivyo wayatumie
kuimarisha ulinzi wa jamii na mali zake.
Ameongeza
kuwa Tanzania haijaweza kufikia kwenye takwimu ya matukio mengi yanayohatarisha
amani hivyo ni vyema kwa misingi iliyopo kuilinda amani wahitimu wakayasimamie
kwa kuwasaidia wananchi na sio kwenda kuwa chanzo cha vurugu.
Awali katika Risala ya wahitimu hao wamesema kumekuwa na
mwamko mdogo kwa wananchi kushiriki mafunzo ya uaskari mgambo kitendo ambacho
kichangiwa.
0 Comments