Shirika la kibinaadamu la Human Rights Watch linasema kuwa vikosi vya
usalama ini DR Congo vimewaua takriban watu 34 wakati wa maandamano wiki hii.
Mazungumzo
yanayoendeshwa na kanisa katoliki yanaendelea mjini Kinshasa ,ili kujaribu
kumaliza mgogoro katika ya upinzani na rais Joseph Kabila ambaye alikataa
kuondoka madarakani wakati muda wake ulipokamilika siku ya Jumatatu.
Kuna ripoti tofauti kwamba watu wengine 17 wameuawa kaskazini
magharibi mwa Congo.
Maafisa wa polisi
wanadaiwa kukabiliana na wanachama wa kundi moja la madhehebu linaloamini
kwamba mwisho wa utawala wa Kabila ndio mwanzo wa mwisho wa dunia.
Wakati huohuo
Mamlaka nchini DRCongo imewakamata watu kadhaa katika mji wa pili kwa ukubwa
nchini humo, Lubumbashi.
Meya wa mji huo
anasema kwamba wanajeshi walikuwa wakiwakamata wahalifu, japo wenyeji wa mji
huo wanasema waliokamatwa ni vijana wanaoshukiwa kupinga utawala wa rais Joseph
Kabila.
0 Comments