Ndege mbili mpya za Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) aina ya
Bombardier Q400 zinatarajia kuanza kazi wakazi wa mikoa ya Mwanza, Arusha
na Zanzibar watakuwa wa kwanza kupata ofa.
Ofisa Habari wa shirika hilo, Lilian Fungamtama amesema
safari mpya za ndege hizo ikiwamo ya Dar es Salaam - Mwanza, nauli
iliyopangwa ni Sh160,000.
Amesema safari za Dar es Salaam - Arusha nauli yake
itakuwa Sh180,00 na Zanzibar - Dar es Salaam ni Sh85,000.
“Ofa hii imetolewa na ATCL kwa safari mpya za ndege hizo,”
alisema Fungamtama.
Amesema hakutakuwa na safari ya moja kwa moja kutoka Dar es
Salaam kwenda Zanzibar, lakini itakuwapo ya kutoka Dar es Salaam -Arusha hadi
Zanzibar.
“Ndege ya kutoka Dar es Salaam kwenda Arusha ndiyo
itakayokwenda kuchukua abiria Zanzibar haitatokea Dar es Salaam moja kwa moja,”
alisema.
Akifafanua kuhusu nauli hizo, Fungamtama alisema
nauli ya kutoka Dar kwenda Kigoma itakuwa katika madaraja mawili ambayo
ilikuwapo tangu awali.
Amesema bado ndege hizo hazijaanza safari katika mikoa yote hadi
hapo watakapotangaza.
Akizungumzia safari za nje ya nchi, alisema itakuwapo ya kutoka
Dar es Salaam - Hahaya hadi Comorro ambayo nauli yake ni Sh543,950 kwenda na
Sh926,650 kwa kwenda na kurudi.
“Lengo letu ni kutoa huduma nzuri itakayomridhisha kila
mteja,” alisema Fungamtama.
0 Comments