LEO OLD TRAFFORD MAN UNITED v MAN CITY!
EFL CUP
Raundi ya 4
Jumanne Oktoba 25
Arsenal 2 Reading
0
Bristol City 1 Hull
2
Leeds 1 Norwich 1 [2-2
baada Dakika 120, Leeds Penati
3-2]
Liverpool 2 Tottenham
1
Newcastle 6 Preston
0
Liverpool wameibwaga
Tottenham 2-1 katiika Mechi ya Raundi ya 4 ya EFL CUP ambalo ndio Kombe la Ligi
huko England katika Mechi iliyochezwa Uwanjani Anfield hapo Jana na kutinga
Robo Fainali.
Bao za Liverpool kwenye
Mechi hii zote zilifungwa na Daniel Sturridge katika Dakika za 9 na 64 na lile
la Tottenham kuingizwa Dakika ya 76 kwa Penati ya Janssen.
Huko Emirates, Arsenal
nao wameingia Robo Fainali baada ya kuipiga Reading Bao 2-0 zote zikifungwa na
Alex Oxlade-Chamberlain.
Hull City, wakicheza
Ugenini, wameingia Robo Fainali kwa mara ya pili mfululizo Jana walipoitoa
Bristol City 2-1 na kwa Bao za Harry Maguire na Michael Dawson huku Bristol
wakifunga Bao lao kupitia Tomlin.
Newcastle wametinga Robo
Fainali kwa kishindo kwa kuinyuka Preston Northen 6-0 kwenye Mechi iliyochezwa
Saint James Park na Wafungaji Bao hizo ni Aleksandar Mitrovic, Bao 2, Mohammed
Diame, Bao 2, Matt Ritchie, kwa Penati, na Ayoze Perez.
Mechi kati ya Leeds
United na Norwich City ilipigwa Dakika 90 na kuwa Sare 1-1 na kisha zikaenda
Dakika za Nyongeza 30 na kuwa 2-2 na mwisho Mikwaju ya Penati Tano Tano ikaipa
Leeds ushindi wa Penati 3-2.
-Msimu huu hili Kombe la Ligi halina Mdhamini na limebatizwa English
Football League Cup, EFL CUP.
-Huko nyuma Kombe la Ligi, kwa sababu za kiudhamini, liliwahi kubatizwa
Coca-Cola Cup, Worthington Cup, Carling Cup na Capital One Cup.
Leo Jumatano zipo Mechi
3 na zote kushirikisha Timu za Ligi Kuu England pekee ambapo Southampton
wataikaribisha Sunderland huko Saint Mary na West Ham kuwa Wenyeji wa Chelsea
kati Dabi ya Timu za London wakati Jijini Manchester ipo Dabi ya Jiji hilo
Uwanjani Old Trafford kati ya Manchester United na Manchester City.
Washindi 8 wa Raundi ya
4 watasonga na kutinga Robo Fainali ambapo Droo yake itafanyika mara tu baada
ya Mechi ya mwisho hapo Jumatano.
Bingwa Mtetezi wa Kombe
la Ligi ni Man City ambao kwenye Fainali Mwezi Februari walitoka Sare 1-1 na
Liverpool na kutwaa Kombe kwa Matuta.
EFL CUP
Raundi ya 4
Mechi zote kuanza Saa 3 Dak 45 Usiku Saa za Bongo isipokuwa inapotajwa
Jumatano Oktoba 26
Southampton v
Sunderland
West Ham v
Chelsea
2200 Man United v Man City
0 Comments