Robby Muhochi Afisa Ustawi wa Jamii Wilaya ya Ikungi.
Mwl Donard Adam Mwalimu wa Shule ya Msingi ya Ikungi.
IKUNGI:
Na Mwandishi wetu.
Afisa Ustawi: Wazazi Hawana Uelewa wa
Kutosha Kuhusu Malezi ya Watoto Wenye Ulemavu
Mwalimu Mlemavu Aeleza Changamoto za
Kufundisha Wanafunzi Maalum Ikungi
Wazazi wengi wenye watoto wenye
ulemavu bado hawana uelewa wa kutosha kuhusu malezi sahihi ya watoto hao, hali
inayochangia changamoto katika ukuaji na maendeleo yao.
Kauli hiyo imetolewa na Afisa Ustawi
wa Jamii wa Wilaya ya Ikungi, Bi. Robby Muhochi, wakati wa mahojiano maalum na
kipindi hiki, kilipotembelea Shule ya Msingi Ikungi, shule ambayo hutoa elimu
kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum pamoja na wasio na ulemavu.
Bi. Muhochi amesema kuwa Halmashauri
ya Wilaya ya Ikungi imejipanga kuwapatia wanafunzi zaidi ya 30 wenye mahitaji
maalum huduma ya bima ya afya, kutokana na uhitaji wao wa huduma za kiafya mara
kwa mara.
"Wanafunzi hawa wanahitaji
uangalizi wa karibu kiafya, hivyo tumeona umuhimu wa kuwapatia bima ya afya ili
kurahisisha upatikanaji wa matibabu."
Kwa upande wake, Mwalimu Donard Adam,
ambaye ni mwalimu mwenye ulemavu anayefundisha katika shule hiyo, amesema
changamoto kubwa wanayokabiliana nayo ni ukosefu wa vifaa vya kufundishia,
hususan kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum.
"Tunayo changamoto kubwa ya vifaa
maalum vya kufundishia, ambavyo ni muhimu sana kwa wanafunzi wetu ili waweze
kujifunza kwa ufanisi."
Mwalimu Donard ameongeza kuwa kuwepo
kwa vifaa hivyo kutasaidia wanafunzi hao kupata elimu bora na yenye usawa kama
ilivyo kwa wengine.
0 Comments