Mkurugenzi wa Shirika la Health Action Promotion Assocciatin (HAPA) Seleman Dandy akiongea na wanahabari katika mradi wa maji katika kijiji cha Matyuku.
SINGIDA
Shirika lisilo la kiserikali la Health Action Promotion Association (HAPA) limetangaza kuwa litatumia zaidi ya shilingi milioni 156 kwa ajili ya uchimbaji wa visima vitatu vya maji katika kijiji cha Matyuku, Wilaya ya Ikungi mkoani Singida.
Meneja wa miradi wa
shirika hilo, Gerald Manyogoto, amesema mradi huo ni sehemu ya juhudi za
kusaidia jamii kupata maji safi na salama, huku shirika likishirikiana kwa
karibu na Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi kuhakikisha changamoto ya maji
inapungua vijijini.
“Tunafanya
kazi kwa kushirikiana na serikali za mitaa ili kuboresha maisha ya wananchi
kupitia miradi ya maendeleo. Maji ni moja ya kipaumbele chetu,” amesema
Manyogoro.
Kwa upande wake, Eric
Poul, Meneja wa kampuni ya N&S Ground Water Tanzania inayotekeleza
uchimbaji huo, amesema kuwa tayari visima viwili vimekamilika na kazi ya
kujenga miundombinu ya usambazaji maji itaanza hivi karibuni.
“Kazi inaendelea
vizuri, tunatarajia kuanza ujenzi wa miundombinu mingine ili wananchi waanze
kunufaika na huduma ya maji,” amesema Poul.
Mkurugenzi wa shirika
la HAPA, Seleman Dandy, amesema shirika hilo sasa linaendesha miradi saba ya
maendeleo, ikiwemo afya, elimu, maji, usafi wa mazingira, utawala bora,
mabadiliko ya tabianchi na ujasiriamali wa kijamii.
“Tunataka
kuona jamii ya Singida inakuwa na maendeleo ya kweli yanayogusa maisha yao ya
kila siku,” amesema Dandy.
Mradi huu unatarajiwa
kunufaisha mamia ya wakazi wa Matyuku na maeneo jirani, na ni sehemu ya dhamira
ya shirika hilo kusaidia jamii kufikia maendeleo endelevu.
Kwa habari
zaidi kuhusu miradi ya maendeleo mkoani Singida, endelea kufuatilia ukurasa
wetu!
#SingidaYetu #MajiNiUhai
#MaendeleoVijijini #HAPA #Ikungi
#RadioSingida #VisimaVyaMaji #CommunityDevelopment #MajiSafinaSalama
0 Comments