Ikungi
Na Mwandishi wetu
Mkazi wa kijiji cha mtunduru kata ya
mtunduru wilaya ya ikungi mkoani Singida
Hamza Hamisi (18) amekamatwa na viongozi wa serikali saa
1:00 usiku nyumban chumbani kwake akifanya mapenzi na Mwanafunzi (14) ambae ni mwanafunzi wa kidato
cha pili (ii) .
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa juzi na
mwenyekiti wa kijiji hicho Juma Nkambi kuhusiana na tukio hilo
amesema mwanafunzi huyo alikamatwa usiku mwishoni mwa wiki iliyopita
kwenye chumba cha Hamza wakifanya mapenzi kama kawaida yao huku Hamza akijua kuwa
mwenzake ni mwanafunzi akitendo kitakacho pelekea kumharibia masomo na maisha
na ndoto zake.
Mwenyekiti wa kitongoji cha Masweya Mashariki Alli
Hamisi Lissu akiwa na Afsa Mtendaji wa kata ya mtunduru Oska
mwakakumbila walimkamata Hamza usiku huo baada ya kupata taarifa za
kiintelijensia wakiwa na Mwanafunzi huyo ana kwa ana chumbani kwake wakidaiwa kuvunja
amri ya sita na wamekiri makosa yao.
Imeelezwa watu hao wamekuwa na mahusiano muda mrefu
na wamekiri wenyewe kuwa na mahusiano baada ya kuhojiwa na polisi walipopelekwa
kituoni na Afsa mtendaji wa kijiji cha mtunduru Veronika John wakiwa na baba wa Mwanafunzi huyo, mzee Martin Samweli.
Taarifa zinasema baada ya kukamatwa walifikishwa
kituo cha Afya Sepuka kwa mahojiano na Mtoto huyo wa Shule alifanyiwa vitendo vya kikatili na Hamza yupo rumande
na polisi bado wanaendelea na mahojiano na baadae afikishwe kwenye
vyombo vya sheria.
Mwalimu mkuu wa shule ya Sekondari
Mtunduru Epmat kairra amethibitisha kuwepo kwa taarifa hizo za
mwanafunzi wake kukamatwa mitaani na kufikishwa polisi wakiwa na mshikaji Hamza
Hamisi na mpaka sasa ameng’ang’aniwa na polisi kwa vitendo hivyo baada ya wote
kukiri makosa yao walipokamatwa ana kwa ana na viongozi wa serikali.
Mapema mwaka huu waziri Mkuu Kassimu Majaliwa aliwaonya
vijana wote, wafanyabiashara na walimu kukaa mbali na wanafunzi wa kike
wasikatishwe masomo yao na ndoto zao waache wasome akawaonya vijana yeyote
atakayewakatisha watoto hao masomo watafungwa miaka 30 jela.
0 Comments