MBUNGE wa jimbo la SIngida Mgharibi Elibariki Kingu ameipongeza Serikali inayoongozwa na Rais Dkt Samia kwa kuwapeleka madaktari bigwa 5 kutoka huduma za kiafya kwa wananchi wa sepuka kupitia kituo chao cha afya cha sepuka kinachotoa huduma za kiafya kwa wananchi wote tarafa ya Sepuka na vijiji vya iramba
Mbunge Kingu amemshukuru Raisi Samia kuweza kuwapata madaktari bingwa kwenye jimbo lake ambapo wagonjwa 346 walipata huduma mbalimbali kutoka kwa madaktari hao amesema serikali imeipa hadhi kubwa wilaya ya Ikungi na kituo cha afya Sepuka kwa ujio wa madaktari bigwa na sasa kituo kina vifaa tiba za kutosha, dawa za kutosha na kupewa mashine ya “ultrasound” na ECG wakala mwanzoni havikuwepo katika taarifa yake kwa mwandishi wa habari hizi jana mganga mfawidhi Dkt Kessia Daniel amesema kituo chake kimepokea neema kubwa na heshima kubwa kutoka na ujio wa madaktari hao kituo tayari kimepokea mashine mbili za kisasa, vifaatiba, dawa za kutosha ili kutumika wakati madaktari haowapo matabibu watu, wauguzi nane, mfamasia mmoja, mtaalamu wa usingizi na ganzi mmoja na maabbara ina wataalamu watatu kituo hakina mtaalamu wa mionzi, madaktari wa macho na meno.
Ameendelea kusema kituo chake sasa kina hudumia wagojwa wa idara ya nje OPD 400 hadi 500 kwa mwezi, kinalaza wagojwa 120 kwa mwezi, akina mama 80 wanaojifungua kwa mwezi, na upande wa kiliniki kituo kinapokea akina mama wajawazito na watoto 500 kwa mwezi nah ii ni pamoja na kliniki tembezi.
Mganga mkuu Wilaya ya Ikungi DMO Dkt Dorisila John amewataja madaktari bigwa 5 waliopelekwa kituo cha Sepuka na Wizara ya afya Mkoa ni Dkt Amon Rya Kitimbo daktari bigwa wa maradhi ya watoto na Dkt Rachee Ng’eni Daktari bigwa wa magojwa ya ndani.
Wengine kwa mujibu wa DMO Ikungi ni Dkt Hosiana Maacha daktari wa usingizi na nganzi Dkt Christopher Mngore daktari bigwa wa upasuaji Dkt Dennis Xavery.
Mkurungenzi mtendaji wa Halmashauri ya Ikungi Justice Kijazi amesema ujio wa madaktari hao umeleta neema kubwa ikungi na kituo cha afya Sepuka sambamba na wananchi wake kwa sababu sasa kituo hicho kitaongoza uwezo wake wa kufanya kazi muda wote kama hospitali kubwa.
Kijazi ameishukuru wizara ya afya kwa kuwapeleka madaktari hao kituo cha afya sepuka na kukipa hadhi na wananch wamebufaika kwa ujio wao sasa vifaatiba vipo vingi dawa zipo nyingi na serikali sasa itaongoza majengo mengine na kuongeza madaktari na watumishi wa afya.
Mbunge Kingu alipata nafasi ya kuonana na madaktari hao na kuwapo kwa ujio wao akawataka wafike tena mara nyingine kwasababu huduma zao bado zinahitajika sana kwa watu wengi.
Baadhi ya wananchi wa Sepuka Meja Lumbi Lulu amesema matatizo yake yaliisha muda mfupi sana baada ya kukutana na madakitari hao hivyo amewataka warudi tena naye Nassoro Labia, Omari Soa, Issa Mkuki na Shabni Gunda wamesema hao ni madaktari bigwa hasa na wamefurahi kwa ujio wao Sepuka
=MWISHO=
0 Comments