KAMATI YA BUNGE YATOA USHAURI KWA TARURA .

 

Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge Mhe Dennis Londo akiongea baada ya kutembelea na kukagua Ujenzi wa Daraja la Minyughe lililopo Wialayani Ikungi katika kijiji na kata ya Munyughe liloghalimu zaidi ya Shl Bil 1.5 fedha za Serikali.

Eng Victor Seff Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mjini Nchini Tarura akifafanua jambo katika kikao cha Kamati ya kudumu ya Bunge katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi.


Meneja wa Tarura Mkoa wa Singida  Mhandisi Ibrahim Kibasa akisoma Taarifa ya Tarura ya Mkoa mbele ya kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida.

      Muonekana wa daraja la Minyughe baada ya kukamilika kwa Asilimia 90 mpaka sasa.






Wataalamu kutoka wakala wa barabara za vijijini na Mjini nchini TARURA wametakiwa kuwa wabunifu kwa kuangalia teknolojia mpya zenye ubora na gharama nafuu katika ujenzi wa miundombinu ya barabara.

Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya miundombinu Denis Londo ametoa wito huo wakati wa ziara ya kamati hiyo mkoani hapa ilipofika kukagua miundombinu ya barabara.

 

Pamoja na kamati hiyo kuupongeza wakala huo Mkoa wa Singida kwa utekeleza wa miradi ya barabara hasa katika ujenzi wa daraja la minyughe lililopo wilayani Ikungi Mwenyekiti huyo akatoa wito kwa wataalamu wa TARURA nchini kuwa wabunifu.

Aidha mtendaji Mkuu wa TARURA nchini mhandisi Victor Seif amesema  wamejipanga kuhakikisha wanaendelea kuboresha miundombinu ya barabara ili wananchi waendelee kunufaika kwa kufanya shughuli zao bila vikwazo hasa vinavyohusiana na barabara.

 

Kwa upande wake meneja wa wakala huo Mkoa Mhandisi Ibrahim Kibasa ameziomba Halmashauri kushirikiana na wakala huo katika kutoa Elimu kwa jamii juu ya utunzaji wa miundombinu ya barabara.

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments