Na Mwandishi wetu
KIJANA mmoja mkazi wa Kijiji cha
Mwankoko “A” Kata ya Mwankoko Manispaa ya Singida mkoani Singida Athumani
Jumanne (46) amemuua baba yake mzazi Jumanne Kivendi (71) katika ugomvi wa
kifamilia.
Habari zilizopatikana kutoka
Kijiji hicho zinasema tukio hilo lilitokea tarehe 30 Aprili 2024 saa 2:00 usiku
wakati baba wa kijana huyo alikwenda kwake usiku huo baada ya kusikia mjukuu
wake akilia akipigwa na Athumani, hivyo alikwenda kuuzima ugomvi huo.
Kwa mujibu wa habari zilizotolewa
na Ayubu Ngura zinasema baba yake Mzee Jumanne alipofika kwa mwanae alianzaa
kumfokea Athumani kwa maneno makali na matusi ya nguoni mbele ya familia yake.
Ayubu aliendelea kusema Athumani
baada ya kusikia maneno makali na matusi kutoka kwa baba yake akakumbukia kuwa
wana ugomvi wa ardhi wa mara kwa mara miaka ya nyuma baba huyo alimuua mkewe
ambaye ni mama yake na Athumani na sasa anamtukana matusi ya nguoni mbele ya
familia yake.
Aliendelea kusema baada ya matusi
hayo Bwana Athumani alipata hasira na akamrukia Mzee huyo, akampiga ngumi
mfululizo na kumwangusha chini na kumkaba koo kwa nguvu akaendelea kumshindilia
ngumi akiwa chini mpaka alipokufa.
Habari zinasema baada ya mzee
Jumanne kufariki mwanae alichukua jembe akaenda shambani kwenye eneo la jirani
yake akachimba tuta akambeba baba yake akamtupia ndani ya tuta hilo, akachukua
kiko chake akakiweka pembeni, akachukua majani ya n’gombe ba bati akaweka juu
yake akafunika na siku ya tatu baadae akapanda miche ya viazi juu yake.
Baada ya siku tatu Athumani
alikwenda kwa Mwenyekiti wa Kitongoji Nkingo akampa taarifa kuwa baba yake mzee
Jumanne Kivendi hayupo nyumbani wiki tatu hajui alipo, ameondoka amechukua kiko
chake na nguo zake mpaka sasa haonekani.
Imeelezwa siku ya 10 wananchi wa
eneo hilo walitilia shaka wakaenda kwake kumhoji baba yake amekwenda wapi,
majibu ya Athumani na maelezo yake, pia muonekano wake uliwatia shaka
wakamuuliza kisa cha kulima tuta lile kubwa na kupanda miche ya viazi juu yake
wakati eneo hilo sio lake la mtu mwingine ambaye ni jirani yake.
Alitoa majibu ya maswali hayo
kuwa mke wa mwenye eneo hilo alimpa kibarua, mume wa mwenye eneo akamuuliza mke
wake kwamba atampaje Athumani kibarua bila idhini yake, mke alikataa hapo
wananchi waliondoka wakamuacha lakini minong’ono mingi chini kwa chini ilizidi.
Siku ya kumi na tatu saa 6:00
mchana wananchi wote wa eneo hilo walikusanyika wakaambiana wachukue jembe
waende kwenye tuta hilo wafukue waone kuna nini, wakaanza kufukua, kwanza
wakakutana na harufu kali wakaendelea kufukua wakaupata mkono wa kiko hapo hapo
majibu ya maswali yao wakayapata na mtuhumiwa alikuwepo alipoona hayo akaanguka
chini akazimia masaa mawili mbele ya Mwenyekiti wa Kitongoji na wananchi.
Wananchi wa eneo hilo la Mwankoko
“A” wakaitana wote pamoja na viongozi wao na Diwani wao Imanuel Kiemi na
Mwenyekiti wa Kijiji Bwana Yakobo Muve walifika kushuhudia tukio hilo,
wakishuhudia nguo za mzee huyo, kiko na mwili wake ukiwa ukiwaq umezikwa kwenye
tuta lililopandwa viazi juu yake, hapo hapo wakaita Polisi walifika kushuhudia
tukio hilo na kulichunguza.
Imeelezwa Polisi wakifuatana na
Madaktari kutoka Hospitali ya Wilaya ya Singida baada ya kazi ya ufukuaji wote
kufanyika wakaanza kumhoji Athumani ilikuwaje mpaka amuue baba yake na alitumia
kitu gani kuumua na kisa cha kumuua baba yaek.
Katika majibu yake alisema siku
ya tukio hilo saa 2:00 usiku alikuwa nyumbani kwake akampiga mwanae Kivendi,
babu yake kusikia kilio cha mjukuu wake alifika na kuanza kumfoka na kumtukana
matusi ya nguoni akidai hataki mtoto huyo apigwe naama amepewa jina la ukoo
wake hatakiwi apigwepigwe hovyo.
Athumani anasema baada ya matusi
hayo makali akamrukia mzee huyo akampiga ngumi za ngumi kadhaa akamwaangusha
chini akamkwida shingo akamkaba kwa nguvu akamkandamiza chini akaendelea kumpa
kichapo akiwa chini baadae akamwacha.
Alipoona baba yake hawezi kuinuka,
akiwa chini amenyamaza kimya kumbe muda huo alishakata moto alipoona hivyo
akambeba akachimba shimo hilo akaweka bati na kiko akafukia shimo hilo na siku
tatu baadae akapanda miche ya viazi juu yake.
Athumani ameendela kuliambia
Jeshi la Polisi kuwa mara kwa mara walikuwa na ugomvi na baba yake wa ardhi eka
moja na miaka ya nyuma mzee huyo alimuua mama yake mzazi.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa
Kijiji cha Mwankoko “A” Yakobo Muve amesema Athumani ana mke na Watoto 4 na mji
wake amekiri mbele ya Polisi na wanakijiji wenzake makosa yake yote na
kuyatolea maelezo makosa yake mbele ya viongozi wake na wananchi, Polisi
wakamchukua kwenda kutoa maelezo mengine kuhusiana na tukio hilo na wananchi
wakaendelea na taratibu za mazishi.
Uchunguzi wa Jeshi la Polisi bado
unaendelea juu ya tukio hilo.
0 Comments