Timu ya Dar es Salaam ya Yanga imeedelea
kupata ushindi katika dimba la Sokoine Jijini Mbeya katika mchezo wa ligi kuu
Premer dhidi ya Wajerajera Tanzania Prisons fc ya Jijini Mbeya, katika Mchezo
huo Prisons hawakuwa makini hasa katika eneo la ulinzi kwani walikuwa wakifanya
makossa mengi hasa katika eneo lao ,Walionesha kujiamini kanakwamba wanacheza
na timu yenye kiwango sawa na wao.
Ukiangalia hata goli la Yanga la kuongoza limepatikana kutokana na kukosa
umakini kwa viungo wa timu hiyo Jumanne Elfadhili,Lambart Charles Mussa Haji
baada ya kupoteza muunganika wa tramision ya uanzishwaji wa mashambulizi,kwani
viungo wa Yanga Mudadhiri Yahaya na Faridi Musa na Khalid Aucho walikuwa
wametawala sana eneo hilo katika kipindi hicho cha kwanza.
Mpira wa majalo uliopigwa na Pacome
Zouzoua ulimpita mlinzi Jumanne Elfadhili ambaye aliluka juu kuupigakichwa na
kuukosa na kumkuta Clement Mzinze aliyekuwa nyuma yake na kuunganisha kimiani
katika dk ya 8 ya kipindi cha kwanza huku golikipa wa prison Yona Amasi
alishindwa kuudaka mpira huo.
Goli la pili la Yanga lilikuwa zuli
pia Prisons walifanya shambulizi langoni
kwa Yanga bila kuwa na tahadhali kuwa iwapo mpira ukinaswa tunatakiwa tujilinde
vipi,kama kawaida yake kiungo Khalid Aucho alipiga pasi ndefu ya pembeni kwa
mlinzi wa kulia Yaw Kouassi aliyekimbia mita kadhaa na kupiga kross upande wa
pili mpira uliyomkuta Pacome Zouzoua na kufunga goli la 2 katika Dk 45+4 likiwa ni goli lake la 5 katika msimu
huu.
Kipindi cha pili mwalimu wa Prison fc
Hamad Ally alifanya mbadiliko katika eneo la kiungo Ally Msengi aliingia kuchukua
nafasi ya Mussa Haji jambo ambalo liliongeza uhai kwa Prison,mabadiliko hayo yaliifanya
Yanga kukosa uhai na muunganiko zaidi na kumfaya Khalid Aucho kufanya kazi ya ziada,Dk 58 kipa wa
Yanga Metacha Mnata alipewa kadi nyekundu kwa kumchezea vibaya Samson Mbagula
na mwamuzi wa mchezo huo Alajiga kumpa kadi nyekundu.
Bao la kufutia machozi la Prison
limefungwa na Jeremia juma baada ya mpira wa adhabu iliyosababishwa na Metacha
mpira ambao ulikwenda moja kwa moja kimiyani na kumujacha gorikipa wa Yanga
Abutwalib Mshery aliyengia kuchukua nafasi ya Metacha Mnata kushindwa la
kufanya,
Pamoja na Yanga kuibuka na ushindi wa
mabao 2-1 katika uwanja wa ugenini lakini bado mwalimu gamondi anatakiwa
kuendelea kuiweka sawa timu hiyo kutokana na inavyocheza sasa,Prisons kama
wangekuwa makini wangeweza kupata bao la kusawazisha huku Yanga kwa asilimia
flani wameonekana kuwa na upungufu katika maeneo flani.
0 Comments