RAIS SAMIA ATOA GARI LA WAGONJWA SEPUKA -(W)IKUNGI

                                  

(picha kutoka maktaba yetu)

MGANGA MKUU wilaya ya Ikungi Mkoani Singida (DMO) Dkt Dorisilla ameahidi kuipambania afya wilaya ya Ikungi kwa watu wote kwa kuanzia ukamilishaji wa ujenzi wa majengo ya Zahanati vituo vya afya, Hospitali zake na upelekekali wa vifaa tiba na dawa sambamba na watumishi.

Licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali kuwepo vituo vya kutolea huduma za kiafya kwa wananchi serikali itaendelea kuziondoa moja baada ya nhingine ili wananchi wapate huduma zote za kuafya kwa ukaribu zaidi kwa viwango vinavyotakiwa na taifa.

Mganga mkuu Dkt Dorisilla ameyasema haya  katika makabidhiano ya gari mpya la pili la wagojwa kwa viongozi wa serikali na chama cha ccm na uongozi wa kituo cha afya Sepuka.

Dkt Dorisilla amesema gari hili lenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 190/= litatumika kupunguza vifo na wa mama wajawazito na watoto kwa muda wote na ndio hasa malengo ya serikali ya Rais Samia hata hivyo Mganga huyo amefurahishwa kusikia wananchi wameridhishwa na huduma za kiafya zinazotolewa na watumishi wa kituo hicho.

“Mambo mengi serikali awamu ya sita ya Mama Samia imeyafanya kwa wananchi wake nchi nzima kwa kusogeza kwa ukaribu huduma zote muhimu kwa wananchi hivyo sisi watumishi wa afya tunampangeza sana Rais wetu Mama Samia “MAMA ENDELEA KUTUPIGANIA SISI WATOTO WAKO”.

Dkt Dorisilla ameendele kusema sasa nchi nzima wameanza kumuelewa vizuri Rais wao Samia anataka nini kwao na si hivyo tu na viongozi nao wameanza kwenda na kasi anayoitaka Rais Samia.

DMO Ikungi amewataka akina Mama kukitumia kituo hicho kupata huduma za kiafya zenye uhakika tofauti na mwanzo ambapo akina Mama watumia muda mwingi kupata huduma za waganga wa kienyeji.

“Tiba hizo hazina uhakika huchelewesha muda na mwishowe watu wanapoteza maisha kwa tatizo ambalo lingemalizwa na vituo vya kutolea huduma za kiafya vilivyopo kwenye maeneo ya watu”.Alisema DMO kwa upande wake katibu wa mbuge wa jimbo la Singida Madgaribi Abubakari Munna ameishukuru serikali ya mama Samia kutoa gari jipya la wagojwa kwa ajili ya kutoa huduma za usafiri kwa wananchi tarafa ya sepuka na vijiv vya jirani wilaya ya Iramba nah ii ni kwa sababu serikali yake iko karibu na wananchi wake muda wote.

Mganga Mfawidhi wa kituo cha afya Sepuka Dkt Kessiah Daniel amesema kituo chake kinatoa hudumd za kiafya muda wote na kwa wananchi wote na huduma hizo wananchi wanaridhika japokuwa bado kuna changamoto chache bado zi-po hasa umeme kukatika katika mara nyingi kwa masaa mengi hata hivyo serikali inalijua hilo.

Dkt Kessial anasema katika miaka ya nyuma kituo kilipoanza kilikua kinapokea akina Mama 14 tu kwa mwezi lakini sas kituo kinapokea akina mama 70 kwa mwezi baada ya huduma zake kuboreshwa na kuwa na watumishi wazuri wanaijituma na wenye ujuzi na kazi walizopewa na serikali.

Ameendelea kusema idadi hiyo itaongezeka siku zote hasa baada ya kituo cha afya kufikia malengo yake katika baadui ya majengo yake na wataalamu kuongezeka kusimamia idara zao muhimu watakzo pewa na malengo hasa ya kituo ni kupambania afya wananchi sepuka.

“Gari tulilopewa na serikali ya Rais Samia Suluhu Hassani litapinguza sana vifo vya akina Mama wajawazito na watoto hawatazalia njiani wala wakunga wa jadi hawatatumika kuzalisha akina Mama majumbani litawawapeleka wagojwa na akina mama wajawazito kwenye Hospitali kubwa kwa matibabu”

Diwani wa kata ya sepuka Halima ng’imba (ccm) aliishukuru serikali ya Rais Samia kuwajali wananchi wa tarafa ya Sepuka kwa kutoa gari mpya ili zitoe huduma kwa wagojwa wa kata yake, tarafa na vijii vya jirani vya wilaya ya Iramba amewataka waganga wasimamie vizuri majukumu yao ili wagonjwa wapate matibabu yanayostahili na wananchi waiamini serikali yao walioichagua.

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments