MKUU WA JAMII YA WAMASAI LEIGWANAN ATOA NENO MSIBANI.

                                

Leigwanan Aisack Lekisongo Tuliiomba serikali kupitia  Edward Lowassa itupatie Elimu kwanza ili kujenga kizazi bora kitakacho endeleza mila na desturi ya jamii ya kimasai na tulifanikiwa kwa hilo.                                           

                                

Kikao kizito kikiongozwa na mkuu wa jamii ya kimasai au mungu wa mila yao Leigwanan Aisack Lekisongo Meijao kujadili juu ya mazishi ya kijana wao.




Baada ya kikao hicho sasa ni kula nyama na tafakali ya nini cha kufanya baada ya maziko ya Leigwanan Lowassa
.

Leigwanan Mkuu  Aisack Lekisongo Meijao mkuu Jamii ya Wamasai Tanzania ni Mungu alitupati Lowassa kama kwani alikuwa msaada mkubwa kwetu, kama inavyofahamika jamii ya wamasai wanaishi katika mikoa 14 Tanzania na wengi wao wakaendelea kujifunza na kupenda kusoma baada ya yeye kuiomba serikali kuipa jamii hii kipaumbele haswa katika masuala ya Elimu.

"Lowasa aliitambua jamii ya Wamaasai ina umasikini mkubwa hivyo yeye aliamua kuiomba serikali jamii hiyo ipewe kipaumbele haswa kwenye masuala ya Elimu kwa wale waliomaliza kidato cha nne kujiunga na chuo cha waalimu hadi sasa wengi wao wanawafundisha watoto na wajukuu zetu" 

 Kutokana na changamoto iliyokuwa ya maji katika wilaya ya Monduli Hayati Lowassa aliweza kupambana na kuitafuta Benki  ya dunia ikafadhili mradi wa kuleta maji (W) ya Monduli, alipokuwa. Mbunge pamoja na nafasi ya Waziri Mkuu aliweza kupambania wafugaji wa jamii hiyo  na kuhakikisha kuwa Sehemu za Malisho zinatengwa kwaajili ya mifugo.

Meijo amesema kuwa hayati Lowassa wao kama viongozi wa jamii ya wamaasai wanasema kuwa hajafa bali amelala,,amesema Edward alikuwa Leigwanan ambapo yapo majina ambayo waliweza kumpatia ikiwemo IRMAKAA,ILKLSHIMU,ILTOIP hii yote ni kutokana na kushiriki shughuli zote za kimila kwa heshima kubwa na alikuwa hana ubaguzi jamani kwetu ni pengo kubwa,lala Shujaa.

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments