Jeshi la Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo limetumia ndege za kivita kuwarudisha nyuma waasi wa M23 waliokuwa wameuzingira mji wa Sake uliopo kilometa 27 magharibi mwa mji wa Goma jimboni Kivu Kaskazini.
Taarifa zinasema kuwa watu wasiopungua 7
walijeruhiwa ndani ya kambi moja ya wakimbizi katikati mwa mji huo ambako
hali ya wasiwasi ilitanda hadi Jumatatu jioni.
Mamia ya Watu waliokuwa wameanza kurudi
majumbani mwao mwishoni mwa wiki iliyopita waliuacha tena mji huo wa Sake baada
ya wapiganaji wa M23 kuuzingira.
Vyanzo vya ndani vimeeleza kuwa kundi hilo
linalodaiwa kupata usaidizi wa jeshi la Rwanda lilizidisha mashambulizi yake
kwenye vijiji vya Kihuli, Kimoka na Luhonga kilometa karibu 5 na mji huo ambako
milio ya silaha nzito iliendelea kusikika hadi jana jioni.
Akizungumza na wananchi wa Sake mwanzoni mwa juma hili Peter Chirimwami, gavana wa jijeshi mkoani Kivu Kaskazini
alisema,
“Ikiwapo nimewasili hapa ni kwa ajili ya kuwatolea
pole, juweni kwamba raisi anawawekea matumaini kuhusu Mnusco inabidi kuwa
watulivu sababu mkiwashambulia mtampatia adui ushindi. Kamwe hatuta kubali
mufanye fujo dhidi ya Monusco," alisema Chirimwami.
Mapigano hayo yanayoanza kuukaribia mji wa Goma
yamesababisha watu zaidi ya milioni saba kuwa wakimbizi baadhi ikiwa ni wale
kutoka wilayani Masisi na Rutshuru wanaohangaika sasa kwenye kambi za
wakimbizi.
Ripoti mpya ya Umoja wa
Mataifa, imeonesha kuwa jeshi la Rwanda linalounga mkono waasi wa M23 linatumia
silaha zenye uwezo wa juu kama vile makombora ya kutoka ardhini kwa
kuzidungua ndege za kivita, vifaa vinavyoweza kuwapa uwezo wa kusonga mbele
katika vita mashariki mwa Kongo.
0 Comments