Mkuu wa Mkoa akiongea na wakazi wa kijiji cha Kizonzo.
Mkazi wa kkijiji cha Mgela akiuliza swali kwa mkuu wa Mkoa katika Mkutano uliyofanyika katika kijii cha Mgale wilayani Iramba.
Mkuu wa mkoa wa Singida Pete Serukamba akitoatoa ufafanuzi wa matumizi bora ya matumizi ya Mbolea kwenye Mkutanao katika kijiji cha Mgale.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Iramba Enosent Msengi akitoufafanuzi kwa Mkuu wa Singida
Mkuu wa mkoa Peter Serukamba akitoa ufafanuzi juu ya Ujenzi wa Zahanati ya kijiji cha Mukulu.
.
Mkuu wa Mkoa
wa Singida Peter Serukamba amewataka
wazazi Wilayani Iramba Kuhakikisha wanawapeleka Watoto
wao Shule kwani ni agizo lililo
tolewa na Serikali nchini kuwa watoto wote walifaulu
kujiunga na kidato cha kwanza wanarripoti Shule
walizopangiwa ,
Serukamba alitoa Kauli hiyo katika ziara yake ya kukagua Miradi mbalimbali
ya Maendeleo katika vijiji vya Kisonga, Mkulu, Mgongo, Mseko, Kizozo, Mgela na
Mtoa Wilayani Iramba.
Akiwa katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa alifafanya
mikutano ya hadhara na kuongea na wananchi wa vijji vya Kizonzo na Mtoa kusikiliza kero zao
na kuzitolea ufafanuzi.
Serukamba ametoa wito kwa viongozi
wote kuanzia ngazi ya Kata na Wilaya zote Mkoani Singida kuhakikisha
wanafuatilia na kuhakikisha wanafunzi wote wa shule za Msingi na Sekondari wenye
sifa wanaanza masomo .
Aidha Mkuu wa Mkoa alisema kuwa Mzazi
yoyote atakaye shindwa kumpeleka mtoto wake shule atachukuliwa hatua za
kisheria ikiwa ni pamoja na kukamatwas na kufikishwa katika vyombo vya
kisheria.
0 Comments