CHANZO NI MFUMO JUMUISHI WA HAKI JINAI.

 


                        Das Singida Naima Chondo (katikati)aongoza maandamano ya wiki ya Sheria nchini.


Watumishi wa Mahakama na wadau wa mambo ya kisheria Mkoani Singida wakiwa katika maandamano kuashiria Uzinduzi wa wiki ya Sheria.


Das Singida Naima Chondo akikata utepe wa kuzindua utoaji Elimu juu ya maswala ya Kisheria na Mahakama.


Hakimu Mkazi Mfawidhi Mkoa Singida Alu Nzowa akitoa taarifa juu ya umuhimu wa Haki jinai.


Mgeni Rasimi Naima Chondo akiongea kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Singida baada ya kupokea Maandamano.


Mgeni Rasimi akitembele mabanda ya utoaji Elimu juu ya maswa ya kisheria hapo ni Theresia Mande akiwakilisha wasaidizi wa kisheria.



Mtaalamu  wa mambo ya kijamii kutoka Dawati la Polisi akitoa maelezo juu ya changamoto wanazokutananazo.


Taasisi ya kupambana Rushwa Nchini PCCB Mkoa Singida nao wakitoa Maelezo mafupi kwa mgeni Rasimi.

Mahakimu,Mawakili,na wadau mbalimbali wakifuatilia matukio katika viwanja vya ofisi ya Hakimu mfawidhi mjini Singida.



Mgeni Rasimi Katibu tawala Wilaya ya Singida akiongea katika kituo cha watoto yatima kilichopo Manguamitogho kabla ya kukabidhi Msaada katika kituo hicho mjini Singida.



                                      Wakikabidhi Msaada huo katika kituo hicho cha Upendo.


                                    Baada ya kukabidhi Msaada huo sasa ni picha ya kumbukumbu.

Imeelezwa kuwa  kukosekana kwa Mfumo Jumuishi wa Haki Jinai nchini umesababisha Ucheleweshaji wa Haki na Kuchukua Muda mrefu wa kuendesha Kesi Mahakamani na kusababisha Wananchi kushindwa kufanya shughuli za maendeleo.

 Hakimu Mkazi Mfawidhi Mkoa wa Singida ALU NZOWA NZOWA alisema hayo Mkoani Singida wakati wa Uzinduzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini katika mkoa wa Singida yanafanyika mkoani humo yakijumuisha Utoaji wa Elimu kwa wananchi ili waweze kujua sheria na haki zao.

 Alisema Mifumo ya Utoaji na Upatikanaji wa Haki nchini ni muhimu Kuboreshwa na Kuimarishwa ili iweze kuleta Usawa na Ustawi katika Jamii.

 Aidha alisema maboresho ya kimkakati katika Tasnia ya utoaji haki yanatakiwa kuwa Jumuishi katika kuboresha sera, sheria na kanuni kwenye sekta ya sheria na Mfumo wa makosa ya Jinai nchini.

 Hata hivyo NZOWA alisema wadau wa mahakama wana nafasi muhimu katika mnyororo wa utoaji haki kwa kushirikiana na mahakama katika masuala yanayohusiana na utoaji haki.

 Katibu Tawala Wilaya ya Singida NAIMA CHONDO amewataka wananchi wa mkoa wa Singida kufuata sheria ili kuendelea kuufanya mkoa kuwa na amani na utulivu kwa muda wote.

 Kauli mbiu ya maadhimisho ya Siku ya sheria nchini ni "Umuhimu wa Dhana ya Haki na Ustawi wa Taifa, n

Nafasi ya Mahakama na Wadau katika Kuboresha Mfumo Jumuishi wa Haki Jinai".

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments