Mgeni Rasimi Mosese Machali Mkuu wa Mkalama.akitoa hotuba katika Siku ya Familia ya Polisi mjini Singida
Mgeni Rasimi akiwa kwenye gwaride maalum
zawadi kwa washindi wa mchezo wa mpira wa pete
Uchangiaji damu pia ulikuwepo katika Bonanza hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama MOSSES MACHALI
amewataka wenza wa Askari wa Jeshi la Polisi
kuendelea kuwatia moyo askali hao ili wapate kuwa na utulivu wa akili ili
waweze kutimiza majukumu yao kwa ufasaha na weledi.
Machali alisema hayo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter
Serukamba wakati akizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya Familia ya Kipolisi iliyofanyika mkoani Singida.
Alisema kuwa endapo familia za
askaripolisi hazitakuwa nautulivu ni rahisi kwa askari kushindwa kutimiza
majukumuyao kwa weldi kutokana na kukosa utulivu.
Naye Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa
Singida ACP Stella Mutabihirwa amesema kuwa lengo la Siku ya Familia ya Kipolisi
ni kuimarisha ushikiano na kujenga umoja baina ya askari na familia zao na
jamii kwa ujumla.
Mutabihirwa aliongeza kuwa maadhimishi
hayo huwakutanisha Polisi ili kupeana moyo kutokana na majukumu waliyonayo ya kulinda usalam wa raia na mali zao.
Hata hivyo Mutabihirwa amewataka
wanchi wa mkoa wa singida kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi kufichua
vitendo vya uhalifu na uvunjivu wa amnai kwa kutoa taarifa kila wakati.
Maadhimisho hayo yaliambatana na kufanyika
kwa bonanza la michezo Mbalimabali ikiwemo
mpira wa miguu, mpira wa pete, riadha, Kufukuza kuku na Burudani
mbalimbali.
0 Comments